Ujerumani yahitaji washirika kutoa jibu la pamoja kuhusu Navalny, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 1:00 pm

September 3, 2020

Ujerumani itajiunga na washirika wake kutoa jibu la pamoja baada ya kupata ushahidi usio shaka wa shambulio la sumu dhidi ya mpinzani nchini Urusi Alexei Navalny, ambaye anapatiwa matibabu katika kitengo cha watu mahututi mjini Berlin. Mkuu wa kamati ya bunge la Ujerumani inayohusika na masuala ya mambo ya kigeni, Norbert Roettgen, ametoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuchukua msimamo wa pamoja wa wazi na mkali kuhusu suala hili. Amekiambia kituo cha televisheni ya taifa la Ujerumani ARD jana jioni kuwa kwa mara nyingine tena tumeshuhudia ukatili ambao una hali halisi ya unyama katika utawala wa rais Vladimir Putin. Alikuwa akizungumza masaa kadhaa baada ya serikali ya Ujerumani kutangaza kuwa Navalny amekuwa mhanga wa shambulio, akielezea matokeo ya vipimo vya mwili kuwa na sumu vilivyofanywa na jeshi la Ujerumani ambavyo vimegundua kemikali inayoathiri mishipa ya fahamu katika kundi la kemikali za Novichok katika mwili wa Navalny.,

Ujerumani itajiunga na washirika wake kutoa jibu la pamoja baada ya kupata ushahidi usio shaka wa shambulio la sumu dhidi ya mpinzani nchini Urusi Alexei Navalny, ambaye anapatiwa matibabu katika kitengo cha watu mahututi mjini Berlin. 

Mkuu wa kamati ya bunge la Ujerumani inayohusika na masuala ya mambo ya kigeni, Norbert Roettgen, ametoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuchukua msimamo wa pamoja wa wazi na mkali kuhusu suala hili. 

Amekiambia kituo cha televisheni ya taifa la Ujerumani ARD jana jioni kuwa kwa mara nyingine tena tumeshuhudia ukatili ambao una hali halisi ya unyama katika utawala wa rais Vladimir Putin. 

Alikuwa akizungumza masaa kadhaa baada ya serikali ya Ujerumani kutangaza kuwa Navalny amekuwa mhanga wa shambulio, akielezea matokeo ya vipimo vya mwili kuwa na sumu vilivyofanywa na jeshi la Ujerumani ambavyo vimegundua kemikali inayoathiri mishipa ya fahamu katika kundi la kemikali za Novichok katika mwili wa Navalny.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *