Ujerumani yaadhimisha miaka 30 ya muungano,

October 3, 2020

Ujerumani leo inasherehekea miaka 30 ya kuungana tena kwa iliyokuwa Ujerumani Mashariki na Magharibi lakini hakutakuwa na shamra shamra kubwa kutokana na janga la virusi vya corona. 

Kansela Angela Merkel na rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier watahudhuria sherehe rasmi za siku ya muungano ambazo mwaka huu zinafanyika kwenye mji wa historia wa Potsdam, kiasi kilometa 25 kusini magharibi ya mji mkuu, Berlin. 

Kwa karibu mwezi mzima matukio kadhaa yamefanyika kuadhimisha miongo mitatu ya kuungana tena kwa Ujerumani mbili mnamo mwaka 1990 miezi michache tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin na kumalizika kwa enzi ya Vita Baridi. 

Kiongozi wa uliokuwa Muungano wa Kisovieti, Mikhail Gobachev amesema sherehe za leo ni ishara kuwa migawanyiko barani Ulaya imedhibitiwa na kukumbusha kuwa mchakato wa kufikia hatua hiyo ulikuwa mgumu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *