Uingereza yakataa mwito wa EU kuubatilisha mswada wa Brexit, on September 11, 2020 at 1:00 pm

September 11, 2020

Baada ya mazungumzo ya dharura mjini London, Umoja wa Ulaya umeonya kuwa mswada mpya wa Uingereza kuhusu biashara utakuwa ukiukaji mkubwa sana wa mpango wa Brexit. Umoja wa Ulaya umesema jaribio la Uingereza kutaka kuidhinisha Mswada wa Soko la Ndani, ambao utaweza kuipa nguvu za kuubadilisha mpango wa Brexit umeharibu kwa kiasi kikubwa uaminifu kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya ukiongeza kuwa ni jukumu la Uingereza kurejesha uaminifu huo. Miongoni mwa maswala mengine, Umoja wa Ulaya unadai mswada huo mpya utahujumu kile kinachojulikana kama makubaliano ya Ijumaa Njema ambayo yalimaliza miongo kadhaa ya machafuko Ireland Kaskazini.,

Baada ya mazungumzo ya dharura mjini London, Umoja wa Ulaya umeonya kuwa mswada mpya wa Uingereza kuhusu biashara utakuwa ukiukaji mkubwa sana wa mpango wa Brexit. 

Umoja wa Ulaya umesema jaribio la Uingereza kutaka kuidhinisha Mswada wa Soko la Ndani, ambao utaweza kuipa nguvu za kuubadilisha mpango wa Brexit umeharibu kwa kiasi kikubwa uaminifu kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya ukiongeza kuwa ni jukumu la Uingereza kurejesha uaminifu huo. 

Miongoni mwa maswala mengine, Umoja wa Ulaya unadai mswada huo mpya utahujumu kile kinachojulikana kama makubaliano ya Ijumaa Njema ambayo yalimaliza miongo kadhaa ya machafuko Ireland Kaskazini.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *