Uingereza yabatilisha hatua ya kumtambua kiongozi wa upinzani wa Venezuela kama rais,

October 5, 2020

 

Mahakama ya rufaa mjini London leo imebatilisha uamuzi wa kumtambua kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Gaido kama rais katika sehemu ya mzozo unaohusiana na kutolewa kwa hifadhi ya dhahabu ya thamani ya dola bilioni moja. 

Jopo la majaji watatu lilipindua uamuzi wa mahakama kuu wa mwezi Julai uliosema kuwa serikali ya Uingereza inamtambua kwa sauti moja Guaido kama rais wa taifa hilo la Amerika ya Kusini. 

Uamuzi huo ulijiri wakati wa mzozo wa zaidi ya dola bilioni moja ya hifadhi ya dhahabu ambapo benki kuu ya Venezuela inataka itolewe kutoka benki ya Uingereza kusaidia kufadhili nchi hiyo katika vita dhidi ya janga la virusi vya corona. 

Mahakama hiyo ya rufaa imesema ilikuwa imeziagiza mahakama za Uingereza kufanya uchunguzi wa kina kutathmini iwapo serikali ya Uingereza inatambua kwamba rais Nicolas Maduro bado anaendeleza mamlaka ya mkuu wa nchi na mkuu wa serikali nchini Venezuela.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *