Uingereza, Umoja wa Ulaya kuongeza juhudi mazungumzo ya Brexit,

October 4, 2020

 

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, wamekubaliana kuongeza juhudi katika mazungumzo ya Brexit ili kuziba “mapengo makubwa” yanayozuia kupatikana maafikiano ya ushirikiano wao mpya wa kibiashara. 

Viongozi hao wawili wamesema mazungumzo ya wiki hii yenye lengo la kupata makubaliano mapya, ya baada ya Brexit kutoka 2021yamewasaidia kupiga hatua lakini bado hakujapatikana muafaka. 

Umoja wa Ulaya umesema makubaliano lazima yafikiwe mwishoni mwa mwezi – au mwanzoni mwa mwezi Novemba. Viongozi hao wawili waliwaagiza washauri wao wa Brexit, Michel Barnier na David Frost, kufanya kazi kwa bidii ili kuziba mapengo hayo yaliyobakia. 

Inakadiriwa kwamba biashara yenye thamani ya matrilioni ya euro kila mwaka itakuwa hatarini ikiwa watashindwa kupata makubaliano.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *