Uingereza inapanga kuwanyima hifadhi wahamiaji haramu,

October 4, 2020

 

Serikali ya Uingereza imesema haitotoa hifadhi kwa wahamiaji wanaovuka bahari kwa boti na kuingia nchini humo kwa njia haramu, kulingana na ripoti za gazeti la Sunday Times. 

Chini ya sheria mpya ambazo zitazinduliwa na waziri wa mambo ya ndani Priti Patel hii leo, serikali ya Uingereza itawasilisha muswada mpya kuhusu mipaka yake ambao utaainisha mpango wake wa kuwashughulikia wahamiaji kwa namna tofauti iwapo watakuwa wameyalipa makundi ya kihalifu kuwaingiza nchini humo. 

Njia mpya na halali za kuingia nchini humo zitaundwa kwa wale ambao wako hatarini. Na wahalifu wa kigeni na wahamiaji wengine wanaotafuta hifadhi ambao hawako hatarini watarudishwa walikotoka. 

Patel amesema kwa sasa kila mtu anaekuja Uingereza na kuomba hifadhi anashulukiwa bila kujali njia aliyoitumia kuingilia nchini humo, na njia hiyo sio sahihi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *