Uingereza, EU wafanya mazungumzo ya dharura kuhusu Brexit, on September 10, 2020 at 5:00 pm

September 10, 2020

Maafisa wa Uingereza na wa Umoja wa Ulaya wanafanya mazungumzo ya dharura mjini London leo, wakati Uingereza ikikosolewa kwa kuwasilisha muswada wa sheria wenye vipengele vinavyokiuka makubaliano juu ya kuondoka kwake katika Umoja wa Ulaya, maarufu kama Brexit.Spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi, amesema Uingereza isahau kufikia makubaliano yoyote ya kibiashara na Marekani iwapo itaendelea na muswada huo. Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza John Major, amemshutumu waziri mkuu wa sasa Boris Jonhson kutaka kuitia doa sura ya Uingereza mbele ya dunia.Lakini waziri wa nchi hiyo anayehusika na mchakato wa Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya, Michael Gove, ameliambia bunge mjini London kwamba baada ya Uingereza kuendeshwa chini ya sheria za kibiashara za Umoja wa Ulaya kwa miaka 40 iliyopita, muswada unaoleta utata unahitajika kama msingi wa utendaji kazi kwa siku za usoni.,

Maafisa wa Uingereza na wa Umoja wa Ulaya wanafanya mazungumzo ya dharura mjini London leo, wakati Uingereza ikikosolewa kwa kuwasilisha muswada wa sheria wenye vipengele vinavyokiuka makubaliano juu ya kuondoka kwake katika Umoja wa Ulaya, maarufu kama Brexit.

Spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi, amesema Uingereza isahau kufikia makubaliano yoyote ya kibiashara na Marekani iwapo itaendelea na muswada huo. Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza John Major, amemshutumu waziri mkuu wa sasa Boris Jonhson kutaka kuitia doa sura ya Uingereza mbele ya dunia.

Lakini waziri wa nchi hiyo anayehusika na mchakato wa Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya, Michael Gove, ameliambia bunge mjini London kwamba baada ya Uingereza kuendeshwa chini ya sheria za kibiashara za Umoja wa Ulaya kwa miaka 40 iliyopita, muswada unaoleta utata unahitajika kama msingi wa utendaji kazi kwa siku za usoni.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *