Ugunduzi kwamba huenda kuna chembechembe za uhai katika sayari ya Venus

September 16, 2020

Dakika 14 zilizopita

Venus

Maelezo ya picha,

Sayari ya Venus: Phosphine inayohusishwa na uhai imegunduliwa

Wazo kwamba viumbe wanaoishi wanaelea katika mawingu ya sayari ya venus ni uwezekano uliopo.

Lakini hilo ni kwa mujibu wa wataalamu wa angani baada ya kugundua kitu kilichopo angani ambacho hakiwezi kuelezeka.

Ni gesi kwa jina Phosphane PH3, molekyuli ilioundwa kutokana na atomu moja ya Phosphorous na tatu za Hydrogen.

Phosphine, ni kitu chenye sumu na chenye harufu mbaya walichokigundua katika mawingu hayo ya sayari ya Venus na ambacho kinaonekana kuwa ishara ya uhai katika sayari hiyo.

Duniani, Phosphine inahusishwa na uhai. Inapatikana katika viumbe vidogo vinavyoishi katika koo za wanyama kama vile Pingu ama maeneo yenye mazingira duni ya hewa kama vile vidimbwi vya maji ardhini. Ni gesi inayoweza kuzalishwa katika viwanda.

Hivyo basi tunauliza ni kwanini gesi hii ipo yapata kilomita 50 kutoka ardhini?

Profesa Jane Greaves wa chuo kikuu cha Cardiff na wenzake wanauliza swali kama hilo.

Na wamechapisha taarifa katika jarida la asili ya anga zinazoelezea ugunduzi wao kuhusu Phosphine katika sayari ye Venus, pamoja na uchunguzi waliofanya ili kujaribu kuonesha kwamba molekyuli hii inaweza kuwa na chanzo asilia na kisicho cha kibaiolojia. Lakini kwa sasa wamechanganyikiwa.

Phosphine

Maelezo ya picha,

Ni gesi kwa jina Phosphane PH3, ni molekyuli ilioundwa kutokana na atomu moja ya Phosphorous na tatu za Hydrogen.

Juu ya kila kitu kinachojulikana kuhusu sayari, hakuna aliyefanikiwa kuelezea chanzo cha Phosphine kibaiolojia. Na sio hata kwa kiwango kilichogunduliwa.

Hii ina maana kwamba ni vyema kugundua kwamba kuna ishara za uhai katika sayari hiyo.

”Tangu niaze kazi yangu nimekuwa na hamu kujua iwapo kuna uhai katika maeneo mengine ya ulimwengu, hivyobasi nafurahi kwamba hilo linawezekana” , alisema Profesa Greaves.

Lakini ni kweli tunawashinikiza watu wengine kutuambia kile ambacho huenda tumekikosa. Stakhabadhi zetu pamoja na data ziko wazi – hivyo ndivyo jinsi sayansi inavyofanya kazi.

Artwork of Venus

Maelezo ya picha,

Sayari ya Venus haipo katika orodha ya uwezekano wa uhai katika maeneo mengine ya mfumo wa sayari

Je ni lipi la kuvutia?

Sayari ya Venus haipo katika orodha ya uwezekano wa uhai katika maeneo mengine ya mfumo wa sayari. Ikilinganishwa na dunia, ni jahanam.

Asilimia 96 ya anga yake ina gesi ya kaboni. Kiwango cha joto katika sakafu yake ni zaidi ya nyuzi 400.

Vifaa vya angani vilivyotua katika sayari hiyo vimechukua dakika chache kabla ya kuharibika.

Hatahivyo umbali wa kilomita 50 kaskazini viwango vya joto sio vya juu.

Hii ndio sababu inaaminika kwamba iwapo kuna uhai katika sayari ya Venus basi ni katika eneo hili.

Soviet probes
Maelezo ya picha,

Wataalamu wa anga za juu waliofika eneo hili walifanikiwa kupiga picha kidogo

Je ni kwanini tunapaswa kuwa na hofu?

Mawingu yake ni mazito na yanamiliki kati ya asilimia 75 hadi 95 za tindi kali ya Sulphuric, ambayo ni hatari kwa viumbe vinavyoishi duniani.

Je ugunduzi huo umepokelewaje?

Kundi hilo lina wasiwasi, likisisitiza kuwa halijadai kwamba limepata uhai katika sayari ya Venus, lakini lina sema kwamba wazo hilo linahitaji kuchunguzwa zaidi kwa kuwa wanasayansi pia wanasaka njia za kibaiolojia ama hata za kikemikali ili kulielezea.

Alma dishes

Maelezo ya picha,

Ishara ya kuwepo kwa phosphine ilithibitishwa na kifaa cha kupiga picha angani cha ALMA telescope nchini Chile

Je hilo litatatuliwa vipi?

Kwa kutuma kifaa kwenda kufanya uchunguzi hususan anga ya sayari ya Venus. NASA hivi majuzi iliwauliza wanasayansi , kufanyia kazi ujumbe utakaokwenda mwaka 2030.

Roboti za kutumia anga zimependekezwa kusafiri kupitia mawingu ya Venus. Urusi ilifanya hivyo kwa kutumia kibofu mwaka 1985.

Artwork of Venus balloon

Maelezo ya picha,

Artwork: One of the best ways to resolve the uncertainty would be with instrumented balloons

Source link

,Dakika 14 zilizopita Chanzo cha picha, JAXA/ISAS/Akatsuki Project Team Maelezo ya picha, Sayari ya Venus: Phosphine inayohusishwa na uhai imegunduliwa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *