Uganda kuwatoa hospitali wagonjwa wa Covid-19 bila kupimwa,

October 2, 2020

 

Wizara ya Afya ya Uganda imefanyia marekebisho muongozo wake wa kukabiliana na corona ambayo itawafanya wagonjwa wa Covid-19 wasioonesha dada ya maambukizi kutolewa hospitalibila kufanyiwa tena uchunguzi.

Wiziri wa Afya Jane Ruth Aceng amesema watu waliotengwa kwa siku 10 watatolewa hospitali ikiwa hawataonesha dalili ya maambukizi.

Hii itapunguza msongamano wa wagonjwa wanaosubiriwa kufanyiwa uchunguzi tena kabla ya kutolewa hospitali.

Awali wagonjwa walikuwa hawawezi kutolewa hospitali hadi wapimwe mara mbili kuhakikisha hawana virusi vya corona. Lakini baadhi yaowalilalamikia muda waosubiri kufanyiwa vipimo hivyo vya lazima licha ya kuwa hawaoneshi dalili ya kuwa wagonjwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *