Ufaransa yatoa wito kwa jeshi la mapinduzi nchini Mali ”uharakisha” ubadilishanaji wa mamlaka, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 30, 2020 at 5:00 pm

August 30, 2020

Ufaransa leo imetoa wito kwa jeshi la mapinduzi nchini Mali ”kuharakisha” maandalizi ya kurejesha uongozi kwa raia baada ya mapinduzi ya mwezi huu na kuonya kuwa mzozo wa kisiasa utawanufaisha wanamgambo.Mapinduzi hayo dhidi ya serikali ya rais Ibrahim Boubakar Keita yaliishtua Ufaransa ambayo ni mshirika wa Mali inayohofia kuwa hali ya kukosa udhibiti nchini humo itahujumu kampeini za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali katika eneo la Sahel lililoko Afrika Magharibi.Waziri wa majeshi wa Ufaransa Florence Parly ameliambia shirika moja la habari la Ufaransa kuwa ubadalishanaji huo wa uongozi unapaswa kufanywa haraka katika muda wa miezi michache na kwamba iwapo hatua hiyo haitachukuliwa, athari itakayokuwa ni kuwanufaisha wanamgambo hao kwasababu hutumia udhaifu wa serikali na Mali kwa sasa ni taifa dhaifu.Maeneo mengi ya ngome ya Mali yako nje ya udhibiti wa serikali kuu na miaka kadhaa ya mapigano imeshindwa kumaliza shughuli za wanamgambo hao ambazo zimesababisha vifo vya maelfu ya watu tangu mwaka 2012.,

Ufaransa leo imetoa wito kwa jeshi la mapinduzi nchini Mali ”kuharakisha” maandalizi ya kurejesha uongozi kwa raia baada ya mapinduzi ya mwezi huu na kuonya kuwa mzozo wa kisiasa utawanufaisha wanamgambo.

Mapinduzi hayo dhidi ya serikali ya rais Ibrahim Boubakar Keita yaliishtua Ufaransa ambayo ni mshirika wa Mali inayohofia kuwa hali ya kukosa udhibiti nchini humo itahujumu kampeini za kijeshi dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali katika eneo la Sahel lililoko Afrika Magharibi.

Waziri wa majeshi wa Ufaransa Florence Parly ameliambia shirika moja la habari la Ufaransa kuwa ubadalishanaji huo wa uongozi unapaswa kufanywa haraka katika muda wa miezi michache na kwamba iwapo hatua hiyo haitachukuliwa, athari itakayokuwa ni kuwanufaisha wanamgambo hao kwasababu hutumia udhaifu wa serikali na Mali kwa sasa ni taifa dhaifu.

Maeneo mengi ya ngome ya Mali yako nje ya udhibiti wa serikali kuu na miaka kadhaa ya mapigano imeshindwa kumaliza shughuli za wanamgambo hao ambazo zimesababisha vifo vya maelfu ya watu tangu mwaka 2012.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *