Ufaransa yarekodi maambukizi mapya 32,000 ya virusi vya corona,

October 18, 2020

 Wakaazi wa mji mkuu wa Ufaransa Paris na miji mingine minane waliwekewa marufuku ya kutoka nje usiku wa kuanzia jana kama hatua ya kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona. 

Hatua hiyo ilijiri baada ya taifa hilo kurekodi idadi ya juu ya maambukizi mapya ya watu 32,000 kwa siku moja. Kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi hivyo hatari kumewafanya maafisa nchini humo kuweka hali ya tahadhari nchini nzima. 

Wasiwasi wa idadi ya maambukizi kuongezeka umekumba nchi nyingi za Ulaya. Katika Jamhuri ya Czech, jeshi limeanza mipango ya kubadilisha uwanja wa maonyesho ya Prague kuwa hospitali, baada ya kushuhudia ongezeko la zaidi ya maambukizi mapya 10,000 ndani ya siku moja. 

Nchini Ujerumani, kansela Angela Merkel amewahimiza raia wa nchi yake kushirikiana kama walivyofanya kipindi kilichopita ili kuepusha kusambaza ugonjwa. 

Merkel ameonya kuwa nchi itakumbwa na wakati mgumu katika miezi ijayo, isijulikane namna ambavyo msimu wa baridi utakavyokuwa, namna Krismasi itakavyokuwa na vyote vitategemea mienendo ya watu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *