Ufaransa: Vikwazo wa Umoja wa Ulaya vinazingatiwa dhidi ya Uturuki, on September 19, 2020 at 3:00 pm

September 19, 2020

Ufaransa imeunga mkono wito wa Cyprus kwa Umoja wa Ulaya wa kuzingatia kuiwekea vikwazo vikali Uturuki, kama serikali ya taifa hilo haitasimamisha jitihada yake ya utafiti wa mafuta na gesi katika eneo la bahari la mashariki ya Mediterania. Waziri wa Ufaransa anaehusika na mahusiano ya Ulaya Clement Beaune amesema vikwazo vitakuwa miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa na mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya kama Uturuki itaendelea kuhatarisha usalama na uingiliaji wa kimipaka wa mataifa wanachama. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kufanya mkutano wao wa kilele siku chache zijazo wenye lengo la kujadili hatua ya Uturuki ya kutafuta hazina ya mafuta na gesi katika maeno ya bahari ambayo Ugiriki na Cyprus zimekuwa zikisisitiza kuwa ni nchi pekee zenye haki ya kufanya utafiti kwenye eneo hilo.,

Ufaransa imeunga mkono wito wa Cyprus kwa Umoja wa Ulaya wa kuzingatia kuiwekea vikwazo vikali Uturuki, kama serikali ya taifa hilo haitasimamisha jitihada yake ya utafiti wa mafuta na gesi katika eneo la bahari la mashariki ya Mediterania. 

Waziri wa Ufaransa anaehusika na mahusiano ya Ulaya Clement Beaune amesema vikwazo vitakuwa miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa na mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya kama Uturuki itaendelea kuhatarisha usalama na uingiliaji wa kimipaka wa mataifa wanachama. 

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kufanya mkutano wao wa kilele siku chache zijazo wenye lengo la kujadili hatua ya Uturuki ya kutafuta hazina ya mafuta na gesi katika maeno ya bahari ambayo Ugiriki na Cyprus zimekuwa zikisisitiza kuwa ni nchi pekee zenye haki ya kufanya utafiti kwenye eneo hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *