Ufaransa na Uingereza zarekodi idadi ya juu ya maambukizi ya kila siku,

October 4, 2020

 

Ufaransa imerekodi maambukizi mapya ya juu ya virusi vya corona ya takriban 17, 000 na ongezeko la vifo 49 ndani ya siku moja. 

Zaidi ya watu elfu 32 sasa wamefariki nchini humo kutokana na virusi vya corona na zaidi ya watu 606,625 kuambukizwa. Visa vya maambukizi nchini humo viliongezeka kufikia asilimia 7.9 kutoka aslimia 7.7.

Nchini Uingereza wizara ya afya imeripoti maambukizi mapya elfu 13 hii ikiwa idadi mara mbili zaidi ya ile iliyoripotiwa siku ya Ijumaa. 

Serikali ya Uingereza imesema kuwa ongezeko hilo la ghafla limetokana na ”masuala ya kiufundi” yaliosababisha kucheleweshwa kuripotiwa kwa maambukizi ya awali. 

Nchini Ujerumani, takwimu kutoka taasisi ya afya ya Robert Koch zimeonesha kuwa maambukizi yameongezeka kwa 2,279 hii leo. 

Idadi ya vifo pia imeongezeka kwa watu wawili na kusababisha idadi jumla ya vifo kufikia 9529. 

Bara Ulaya liko katikati ya wimbi la pili la kuzuka upya kwa ongezeko la maambukizi huku vikwazo vipya vikiwekwa kote barani humo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *