UEFA wameruhusu mashabiki viwanjani,

October 2, 2020

UEFA wametangaza kuwa wataruhusu mashabiki kuingia uwanjani katika mechi za Champions League na timu ya taifa kwa asilimia 30 ya uwezo wa uwanja kuchukua mashabiki.

Uamuzi huo utatekelezwa endapo sheria za taifa husika hazitakuwa zinazuia, kingine katika michezo hiyo mashabiki wa timu mgeni hawatoruhusiwa kuingia viwanjani kama tahadhari ya Corona.

Hii ni ishara njema na inakuja ikiwa ni miezi takribani saba toka michezo isimame na mashabiki kutoruhusiwa kuingia viwanjani kutokana na kuingia kwa virusi vya Corona katika mataifa ya Ulaya mwezi March 2020.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *