Uchunguzi wafanyika kubaini chanzo cha moto uowaka katika Chuo Kikuu cha Uganda

September 20, 2020

Dakika 1 iliyopita

Moto uliwaka kuanzia majira ya saa sita usiku mpaka asubuhi

Maelezo ya picha,

Moto uliwaka kuanzia majira ya saa sita usiku mpaka asubuhi

Police nchini Uganda wanachunguza chanzo cha moto uliokiteketeza chuo kikuu maarufu, kikubwa na cha zamani zaidi nchini humo cha Makerere, kilichopo matimati ma mji mkuu Kampala.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda moto huo ulianzia kwenye paa, na baadae kusambaa kwenyenye sakafu za majengo ya vitengo vya fedha na rekodi za chuo.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa maafisa walikabiliana na moto mkubwa kuanzia takriban saa sita usiku hadi asubuhi Jumapili.

Jengo maarufu lililoungua mbalo linafahamika kama Ivory Tower, lenye kuta nyeupe na madirisha ya bluu, ni moja ya majengo yanayotambulisha Chuo hicho maarufyu barani Afrika.

Picha katika baadhi ya mitandao ya kijamii ya Chuo hicho zinaonesha sehemu ya nje ya kuta nyeupe za chuo hizo ziungua na kugeuka kuwa rangi nyeusi, na baadhi ya madirisha yaliyoungua:

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Ivory Tower pia lina ofisi ya Naibu Kansela wa chuo hicho pamoja na ukumbi mkuu wa chuo.

Naibu kansela Profesa Barnabas Nawangwe, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter , ameelezea tukio hilo kama asubuhi nyeusi sana na akaongeza kuwa uharibifu uliotokea ni wa kiwango cha kutoaminika.

Makerere ni mojawapo ya vyuo vikuu vya hali ya juu zaidi barani Afrika, na ndicho Chuo Kikuu cha zamani zaidi katika Afrika Masharaiki, ambapo kilianzishwa mwaka 1922 mara ya kwanza kama shule ya ufundi.

Viongozi mbali mbali wa Afrika wamepata elimu ya juu katika Chuo cha Makerere akiwemo muasisi wa Taifa la Tanzania hayati mwalimu Julius kambarage Nyerere.

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, Makerere university/Twitter Maelezo ya picha, Moto uliwaka kuanzia majira ya saa sita usiku mpaka…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *