Uchebe: Nimempa Shilole Talaka Tatu, Akae Eda

September 10, 2020

FUNDI gereji na mfanyabiashara Uchebe amefunguka kinachondelea baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na aliyekuwa mkewe msaniii Shilole, ambapo amesema ametoa talaka za awamu hivyo anamtaka Shilole akae eda ili kupatiwa huduma.Akizungumza na East Africa Radio, Uchebe amesema hawezi kusema kama ndoa ni mbaya kisa yake imeingia dosari kwa sababu ndoa ni jambo la kheri japo kama vijana wanakutana na mambo mengi. “Matatizo yanaponikuta huwa namuomba sana Mungu nisifanye jambo la ajabu, maana wanawake wana vitu viwili kwanza anapomkosea mumewe hakubali anataka kushindana naye na kwenye ndoa ndiyo inawabeba sana,” amesema Uchebe. Aidha, ameendelea kusema; “Mitihani ipo na inatokea ni moja ya hatua kwenye maisha, sasa hivi nimejipunguza kidogo sipo karibu na mwenzangu na nimetoa talaka ambazo zina awamu pia anatakiwa akae heda kupata huduma, ukitaka kuoa kuna misingi mingi unatakiwa kuifuata.”,

FUNDI gereji na mfanyabiashara Uchebe amefunguka kinachondelea baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na aliyekuwa mkewe msaniii Shilole, ambapo amesema ametoa talaka za awamu hivyo anamtaka Shilole akae eda ili kupatiwa huduma.

Akizungumza na East Africa Radio, Uchebe amesema hawezi kusema kama ndoa ni mbaya kisa yake imeingia dosari kwa sababu ndoa ni jambo la kheri japo kama vijana wanakutana na mambo mengi.

 

“Matatizo yanaponikuta huwa namuomba sana Mungu nisifanye jambo la ajabu, maana wanawake wana vitu viwili kwanza anapomkosea mumewe hakubali anataka kushindana naye na kwenye ndoa ndiyo inawabeba sana,” amesema Uchebe.

 

Aidha, ameendelea kusema; “Mitihani ipo na inatokea ni moja ya hatua kwenye maisha, sasa hivi nimejipunguza kidogo sipo karibu na mwenzangu na nimetoa talaka ambazo zina awamu pia anatakiwa akae heda kupata huduma, ukitaka kuoa kuna misingi mingi unatakiwa kuifuata.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *