Uchaguzi Tanzania 2020: Katibu wa kamati ya maadili afafanua adhabu dhidi ya Tundu Lissu

October 5, 2020

Huwezi kusikiliza tena

Dakika 1 iliyopita

Kamati ya kitaifa ya Maadili nchini Tanzania imesisitiza kuwa hatua yoyote ya mgombea urais wa chama kikuu cha Upinzani, CHADEMA Tundu Lissu, kufanya kampeni wakati wa shughuli za kichama ama binafsi, kamati yake inaweza kupendekeza hatua za kuchukuliwa, kwa sheria zingine za nchi, kwa kuwa Mamlaka ya kamati hiyo yanaishia kwenye kumsimamisha.

Ufafanuzi huo unakuja siku moja baada ya Chama hicho kuridhia adhabu ya siku saba ya kutofanya kampeni kwa mgombea wake, Tundu Lissu kwa madai ya kukiuka maadili wakati wa kampeni zake, lakini Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisisitiza kuwa mgombea huyo atapangiwa majukumu mengine, kwa kofia ya Makamu mwenyekiti wa chama.

Ni Mwenyekiti wa CHADEMA, taifa, Freeman Mbowe akielezea kuhusu adhabu ya mgombea Urais wa chama hicho, Tundu Lissu, lakini hili la kumpangia majukumu mengine ya kichama ilhali ana adhabu ya kufungiwa na kamati ya kitaifa ya Kimaadili, limeendelea kugawa wengi nchini humo, je majukumu hayo hayavunji maadili? na Je kamati ya maadili ya kitaifa itakubaliana na hilo?

Awali nimemuuliza hayo katibu wa kamati ya maadili ya kitaifa Emanuel Kawishe, ambaye anaanza kufafanua kuhusu adhabu hiyo iliyotolewa kwaTundu Lissu

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *