Uchaguzi Tanzania 2020: Je, ni elimu bora au bora elimu?

September 12, 2020

  • Humphrey Mgonja
  • BBC Swahili

Dakika 2 zilizopita

elimu

Serikali ya Tanzania  chini ya rais John Magufuli  ilipitisha waraka wa  elimu namba 6 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa elimu bure kwa shule  sekondari.

Waraka huo ulioanza kutekelezwa Januari 2016  umechangia kuinua sekta ya elimu na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza licha ya changamoto kadhaa  kujitokeza. Awali elimu ya msingi ilikuwa ni bure huku shule za secondari ilipiwa ada kiasi cha dolla 17.Ndani ya miaka mitano Serikali ya Tanzania imeshatumia zaidi ya trilioni 1 katika kutekeleza sera ya elimu bila malipo kwa shule za msingi hadi kidato cha nne.

Ripoti iliyotolewa na ofisi ya taifa ya Takwimu imeonesha idadi ya waalimu katika shule za serikali imepungua kwa zaidi ya asilimia tano.”Kwa kweli serikali imejitahidi lakini Serikali iangalie namna yakuongeza walimu na vifaa vya kufundishia ili wanafunzi wanufaike na wapate elimu yenye uhakika”Serikali imeimarisha miundo mbinu kwa kuongeza idadi ya shule za msingi zaidi ya mia tisa na shule za sekondari zaidi ya mia sita  kutoka mwaka 2015.

Hata hivyo changamoto iliyopo ni ongezeko la wanafunzi ambao kwa kidato cha kwanza hadi cha nne idadi yao imekuwa zaidi ya laki tano kutoka mwaka 2015. Wastani wa mwalimu mmoja ni kufundisha wanafunzi 40 kwa shule za sekondari za umma  lakini kwa kujibu wa ripoti ya ofisi ta taifa ya takwimu  ya mwaka 2019 inaonesha ongezeko la wanafunzi limeadhiri uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kwa asilimia 29.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Mafanikio na Changamoto ya ‘Elimu Bila ada Tanzania’

 Baadhi ya wanafunzi wanasema sera hii imekuwa mkombozi kwao kwani kwa sasa wanapata muda wa kutosha kusoma “Imetusaidia hata katika ufaulu Muda ambao tungekuwa tupo nyumbani saivi tunakuwa tupo shuleni tunasoma bila kuwaza kufukuzwa ada”.  Kwa upande wa wazazi wanaona licha ya kuwa na elimu bila ada bado wanahitaji kushirikishwa ili wanafunzi wapate elimu bora na sio bora elimu                           “Serikali imefanya kazi kubwa lakini hizo ruzuku wanazotuma mashuleni nadhani hazitoshi inatupasa sisi wazazi tusssshirikishwe ili kujua hela zinatumikaje na kipi tushirikiane kuwezesha upatikanaji wa huduma nyingine kama chakula, maji, ulinzi na hata mazingira” Wengi wakiridhishwa na hatua ya elimu bila malipo kuanzia awali  hadi kidato cha nne ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014, hata hivyo baadhi ya wadau wa elimu wanaona kipaumbele kinahitajika sasa kwenye ubora wa elimu yenyewe.

Source link

,Humphrey Mgonja BBC Swahili Dakika 2 zilizopita Serikali ya Tanzania  chini ya rais John Magufuli  ilipitisha waraka wa  elimu namba…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *