Uchaguzi Guinea: Kiongozi mwenye umri wa miaka 82 anayetaka kuongoza kwa awamu ya tatu

October 15, 2020

Dakika 25 zilizopita

Alpha Conde alikuwa katika upinzani kwa miaka mingi kabla ya kushinda uchaguzi 2010 na 2015

Alpha Condé, Kiongozi wa Guinea mwenye miaka 82, Jumapili hii anawaomba wapigakura wa nchi yake milioni 5.4 wampigie kura aweze kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu.

Hatua hii inazua wasiwasi kuwa kipindi hiki huenda kikawa cha changamoto kwa Afrika Magharibi.

Ikiwa atashindwa kupata ushindi wa zaidi ya 50% ya kura rais huyo pangine anaweza akaingia kwenye duru ya pili dhidi ya mpinzani wake , Cellou Dalein Diallo, hatua ambayo pengine itasabibisha makabiliano makali kwenye mitaa ya Conakry, mji ulio na watu wengi

Kuingia madarakani kwa Bwana Condé mwezi Disemba mwaka 2010 ulikuwa mchakato wa kwanza wa demokrasia ya kweli ya kukabidhiana madaraka katika historia ya miaka 52 ya uhuru wa nchi yake – baada ya utawala wa kijeshi ambao ulitawaliwa na vitendo vya ukandamizaji na ukatili , tukio la karibuni lilikuwa mauaji ya septemba 28 mwaka 2009, pale vikosi vilipowaua takribani wafuasi wa upinzani 160, na kuwabaka wanawake 110, waliohudhuria mkutano wa hadhara katika uwanja wa taifa.

Mauaji yaliofanyika katika uwanja wa michezo 2009 yanakumbusha ukatili uliofanyika nchini Guinea

The 2009 stadium massacre is a reminder of Guinea’s brutal past

Yeye mwenyewe alitumikia kifungo kwa kumpinga Jenerali Lansana Conte , ambaye alitawala tangu mwaka 1984 mpaka kifo chake mwaka 2008, na alikuwa akikabiliwa na kazi kubwa ya kufanyia mabadiliko vikosi vya usalama na kuijenga nchi katika misingi ya kidemokrasia na uwajibikaji, katika kuheshimu haki za binadamu na uwazi kwenye masuala ya fedha za Umma.

Mafanikio

Miaka 10 iliyopita imekuwa ya maendeleo.

Hofu ya awali ya mapinduzi ya kijeshi ilianza kupungua taratibu, angalau jeshi kwa sehemu lilifanyiwa mabadiliko maafisa wengi walitakiwa kustaafu.

Timu ya mawaziri imeurejesha uchumi katika hali nzuri, na kujenga mahusiano mazuri na Shirika la Fedha duniani (IMF) na jumuia ya wafadhili.

Guinea ina utajiri mkubwa wa madini na udhibiti wa sekta ya uchimbaji imesimamiwa.

Imani kati ya wawekezaji imerejea, ikifungua matarajio kwamba Simandou, mojawapo ya amana kubwa za chuma ulimwenguni, zinaweza kutumiwa mwishowe – kutengeneza maisha mapya ya maelfu ya watu na ujenzi wa reli mpya kuunganisha eneo la kusini lililokuwa limefungwa kuelekea pwani.

Ikiwa ni moja kati ya nchi tatu zilizoathirika vibaya na mlipuko wa Ebola -sambamba na majirani Sierra Leone na Liberia-Guinea ilipata uzoefu wa kupambana na magonjwa ya kuambukiza hatimaye kupata mwanga katka mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Mmoja wa wazee wa siasa za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Bwana Condé alianzisha tena wasifu wa Guinea katika ramani ya kidiplomasia ya Kiafrika.

Changamoto

Bado matatizo makubwa yanaendelea, hasa masuala ya haki za binadamu.

Wapinzani kama vile Bwana Diallo wamekabiliwa na vitendo vya udhalilishaji wakati maisha ya kisiasa bado yana kovu na milipuko ya mara kwa mara ya vurugu za barabarani kati ya waandamanaji wa vijana waliofadhaika na vikosi vya usalama ambavyo, licha ya mafunzo kwa mara nyingine tena, bado mara nyingi hutumia nguvu kupita kiasi ili kuzuia machafuko.

Kwa kuongezea, ahadi ya muda mrefu ya maafisa wa kijeshi kushtakiwa kwa mauaji ya Septemba 28 bado halijatekelezwa, licha ya kampeni endelevu na familia za waathirika, mashinikizo ya kidiplomasia za kigeni na dokezo kwamba Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) itaingilia kati ikiwa Mamlaka ya Guinea itashindwa kuchukua hatua.

Takriban mmoja wa wanajeshi walioshtakiwa rasmi alikuwa ameshikilia ofisi ya serikali chini ya Bwana Condé, wakati Moussa Dadis Camara – mtawala wa jeshi ambaye vikosi vyake vilifanya mauaji hayo – amehojiwa lakini, mwishowe, aliachwa bila shida akiwa uhamishoni huko Burkina Faso.

Kapteni Camara ameendelea kuwa na umaarufu mkubwa katika mji wa makazi yake Guinée Forestière, na wanasiasa waandamizi wanaonekana kusita kuchukua hatua zozote ambazo zinaweza kutishia matumaini ya kupata uungwaji mkono katika eneo hilo.

Katika uchaguzi wa 2015 Bw Diallo aliunda muungano wa ajabu wa uchaguzi na kambi yake, wakati mshirika muhimu wa Kapteni Camara ni waziri mwandamizi katika serikali ya Bw Condé.

Mkanganyiko wa muhula wa tatu

Ni mpambano katika kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, ambao ambao umetokana na uamuzi wa Bw Condé wa kuwania muhula wa tatu – hatua ambayo ilitokana kubadilisha katiba, kupitia kura ya maoni mnamo Machi.

Katiba mpya haijafuta mipaka ya vipindi viwili, lakini awamu za awali hazihesabiki.

Mapema mwaka huu, shirika la kikanda la Ecowas (Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi) liligundua majina milioni 2.5 ya wapiga kura wa kubuni kwenye orodha ya wapiga kura.

Upinzani uliamua kususia kura ya maoni na kumpa njia nyeupe ya mamlaka bwana Conde

Katika siku za hivi karibuni, alisema kuwa haya yalikuwa mabadiliko ya kikatiba ambayo alitamani sana kutekeleza lakini alihisi kuwa hangeweza kuyapa kipaumbele wakati wa miaka ya mwanzo ya utawala wake.

Kulikuwa na maandamano mapema mwaka huu dhidi ya kufanya kura ya maoni ambayo upinzani ulisusia

Maelezo ya picha,

Kulikuwa na maandamano mapema mwaka huu dhidi ya kufanya kura ya maoni ambayo upinzani ulisusia

Ingawa Bwana Condé hakuthibitisha rasmi kwamba atasimama tena, hata mapema mwaka jana azma yake ya kufanya hivyo tayari ilikuwa katika mazungumzo ya kawaida huko Conakry – na chanzo cha wasiwasi kati ya viongozi wengine wa Afrika Magharibi, na wanadiplomasia wa Ulaya, ni kuhofia kuzuka vurugu tena katika nchi yenye historia ndefu kama hiyo ya vurugu za kisiasa za mijini.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *