Uchafu wa mazingira wasababisha asilimia 13 ya vifo barani Ulaya, on September 8, 2020 at 6:00 pm

September 8, 2020

Shirika la ulinzi wa mazingira katika Umoja wa Ulaya limechapisha ripoti yake, inayoonyesha kuwa kati ya vifo vinane katika nchi za umoja huo, kimoja hutokana na sababu za uchafuzi wa mazingira.Ripoti hiyo iliyochapishwa leo inaonyesha kuwa watu wenye kipato cha chini na wale kutoka jamii za pembezoni, ndio walio na hatari kubwa ya kukumbwa na athari za uchafuzi wa mazingira.Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Copenhagen limesema katika ripoti hiyo, kuwa watu wapatao 400,000 hufariki dunia barani Ulaya kila mwaka kutokana na magonjwa yenye uhusiano na mazingira machafu.Aidha, shirika hilo limesema janga la virusi vya corona limeonyesha bayana udhaifu wa wakaazi wa Ulaya mbele ya madhara ya uchafuzi wa mazingira. Miongoni mwa hali za kimazingira zinazowaathiri zaidi maskini ikilinganishwa na watu wenye kipato kizuri, na mawimbi ya joto na majira ya baridi kali.,

Shirika la ulinzi wa mazingira katika Umoja wa Ulaya limechapisha ripoti yake, inayoonyesha kuwa kati ya vifo vinane katika nchi za umoja huo, kimoja hutokana na sababu za uchafuzi wa mazingira.

Ripoti hiyo iliyochapishwa leo inaonyesha kuwa watu wenye kipato cha chini na wale kutoka jamii za pembezoni, ndio walio na hatari kubwa ya kukumbwa na athari za uchafuzi wa mazingira.

Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Copenhagen limesema katika ripoti hiyo, kuwa watu wapatao 400,000 hufariki dunia barani Ulaya kila mwaka kutokana na magonjwa yenye uhusiano na mazingira machafu.

Aidha, shirika hilo limesema janga la virusi vya corona limeonyesha bayana udhaifu wa wakaazi wa Ulaya mbele ya madhara ya uchafuzi wa mazingira. Miongoni mwa hali za kimazingira zinazowaathiri zaidi maskini ikilinganishwa na watu wenye kipato kizuri, na mawimbi ya joto na majira ya baridi kali.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *