Ubosi Unanifanya Nisiolewe, Umri Unazidi Kusonga..Naombeni Ushauri

October 11, 2020

Tangu nimalize harakati za masomo ni miaka 6 sasa. Wenzangu wote niliyokuwa nao ama wameolewa na kupata watoto ama wamepata watoto nje ya ndoa.

Mimi tangu nikiwa mdogo na kwa maadili niliyolelewa niliapa kutokuzaa nje ya ndoa. Lakini mpaka sasa nina miaka 33 sijapata mume wa kunioa.

Mbaya zaidi kwa sasa nina cheo kazini kwangu, basi kila mwanaume ananiogopa. Hapa nauona uzee unasogea sina mume wala mtoto.

Najiuliza, nivunje kiapo changu cha kutokuzaa nje ya ndoa ama niendelee kusubiria mume nisiyejua atapatikana lini na huku umri unaenda?

Niko njia panda jamani naombeni ushauri.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *