Tundu Lissu “Sisi Hatuwezi Kuishi Bila Dunia”, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 3, 2020

Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameahidi kuwa atahakikisha anarudisha mahusiano mema baina ya Tanzania na Dunia nzima.Lissu amesema hayo leo Septemba 2, 2020, akiwa anaendelea na uzinduzi wa kampeni kwa chama hicho kwa Mkoa wa Shinyanga, ambapo amesema nchi ya Tanzania haiwezi kuishi bila ya Dunia.“Katika mambo ya kwanza ambayo tutayafanyia kazi ni kurudisha mahusiano mema na Dunia, sisi hatuwezi kuishi bila Dunia,Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia”, alisema Tundu Lissu.Aidha Lissu amesema kuwa ili kukuza uchumi wa nchi atahakikisha anajenga na kudumisha mahusiano mema na ulimwengu wote, “Serikali yetu katika kukuza uchumi wa nchi, lazima tujenge mahusiano mema na Dunia, hatuwezi kuishi bila Dunia, Dunia inaweza ikaishi bila sisi”.,

Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameahidi kuwa atahakikisha anarudisha mahusiano mema baina ya Tanzania na Dunia nzima.

Lissu amesema hayo leo Septemba 2, 2020, akiwa anaendelea na uzinduzi wa kampeni kwa chama hicho kwa Mkoa wa Shinyanga, ambapo amesema nchi ya Tanzania haiwezi kuishi bila ya Dunia.

“Katika mambo ya kwanza ambayo tutayafanyia kazi ni kurudisha mahusiano mema na Dunia, sisi hatuwezi kuishi bila Dunia,Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia”, alisema Tundu Lissu.

Aidha Lissu amesema kuwa ili kukuza uchumi wa nchi atahakikisha anajenga na kudumisha mahusiano mema na ulimwengu wote, “Serikali yetu katika kukuza uchumi wa nchi, lazima tujenge mahusiano mema na Dunia, hatuwezi kuishi bila Dunia, Dunia inaweza ikaishi bila sisi”.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *