Tume ya uchaguzi yatishia kuwafutia wagombea wenye viashiria vya uvunjifu wa amani,

October 6, 2020

Na Timothy Itembe Mara.

TUME ya Taifa ya uchaguzi imesema kuwa wagombea wenye viashiria vya ufunjifu wa Amani ambao wanakiuka misingi ya uchaguzi huwenda wakafutiwa kushiriki uchaguzi.

Akiongea Mkurugenzi wa uchaguzi,Wilson Mahera kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi ambao ulikalia ndani ya ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa mkoa Mara jana alisema kuwa endapo chama cha siasa na mgombea yeyote atakiuka misingi ya uchaguzi yopo hatarini kufutiwa kushiriki uchaguzi.

“Tume ya Taifa ya uchaguzi kwa mamlaka iliyopewa chini ya ibara 41(4) ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na vifungu vya 358(1)37(1)(a)na 46(1) vya sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343na kifungu cha 48(1)cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa sura ya 292 imetangaza tarehe 28Okotoba 2020 ambayo nisiku ya jumatano kuwa ni siku ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kwa jamuhuri ya muungano na madiwani kwa Tanzania bara na endapo kuna atakaye kiuka misingi hiyo tume inaweza kumfutia kushiriki uchaguzi”alisema Mahera.

Mkurugenzi huyo aliongeza kusema kuwa kwa mjibu wa kifungu cha 124Acha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343 Tume kwa kushirikiana na serikali na vyama vya siasa iliandaa maadili ya uchaguzi ya mwaka 2020 vyama vya siasa vilishirikishwa kwa kupewa frusa ya kutoa maoni katika rasimu zilizokuwa zikiandaliwa kwa hali hiyo kama kuna chama cha siasa ama mgombea atakiuka atakuwa anafanya makusudi na tume haitasita kumchukulia hatua.

Kwa upande wake Jaji mstaafu,Thomas Mihayo alisema kuwa Tume imekuwa inasisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeni zao ikiwemo kuepuka lugha za kashifa namenmo ya uchochezi yanayotishia usalama na Amani ya nchi.

Pia kuhakikisha kuwa wanaepuka kufanya kampeni ambazo zinaashiria ubaguzi katika misingi ya jinsia walemavu,ukabila,udini,maumbile au rangi tunaendelea kuwasisitiza vyama na wagombea kuwa wanapokuwa na malalamiko yoyote ya kimaadili basi hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya mda uliopangwa aliongeza kusema Jaji.

Jaji alimaliza kwa kusema kuwa Tume inawahakikishia wananchi kuwa imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba sheria Kanuni na miongozo mbalimbali na inaamini kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu watanzania wataweza kupiga kura kwa amani na siku ya uchaguzi.

Jaji huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wadau wote waliohudhuria semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania kupekela ujumbe kataika maeneo mbalimbali wanayotoka ili wananchi nawapiga kura wajitokeze kwa wingi kupiga kura ambayo nihaki ya kikatiba kwa kila moja aliye na sifa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *