Trump na mkewe waambukizwa virusi vya corona

October 2, 2020

Trump mwenye umri wa miaka 74 yuko katika kundi la watu wanaoaminika kuwa wanaweza kuathirika vibaya na virusi hivyo, kwanza kutokana na umri wake na pili kwa kuwa anadaiwa kuwa na uzani kupita kiasi. Rais huyo amekuwa na afya njema katika kipindi chote ambapo amekuwa rais ila hafanyi mazoezi ya mara kwa mara au kula chakula chenye afya. Awali Trump alipuuza virusi hivyo na mara kadhaa amenukuliwa akisema kwamba virusi hivyo vitaangamia tu. Zaidi ya watu laki mbili wamefariki kutokana na virusi vya corona Marekani huku idadi kubwa ikiwa wazee na watu waliokuwa na magonjwa mengine kabla ya kuvipata virusi hivyo.

 

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *