Trump kuondoa wanajeshi Afghanistan na Iraq,

October 9, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mpango wa kupunguza idadi ya wanajeshi walioko nchini Afghanistan ifikiapo tarehe 25 Desemba.

Trump alitoa maelezo hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema, ‘‘Wanajeshi wetu wanaohudumu Afghanistan wanastahili kuwa majumbani mwao kipindi cha sherehe za Krismasi.’’

Katika mazungumzo aliyofanya mnamo tarehe 10 Septemba na waandishi wa habari White House, Trump alisema, ‘‘Tutapunguza idadi ya wanajeshi wetu wanaohudumu Afghanistan hadi 4000. Kwa utaratibu huo huo, pia tutapunguza wanajeshi waliokuwa Iraq hadi 2000.’’

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *