Trump, Biden wakwaana kuhusu mabadiliko ya tabianchi, on September 15, 2020 at 8:00 am

September 15, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine amekanusha mchango wa mabadiliko ya tabia nchi katika ongezeko la mioto ya msituni inayoteketeza misitu magharibi mwa nchi yake, akisema bila kunukuu ushahidi wowote wa kisayansi kuwa viwango vya joto duniani vitaanza kushuka. Badala yake, Trump amesema tatizo kuhusiana na mioto hiyo sio mabadiliko ya tabianchi, bali ni utunzaji mbaya wa misitu. Gavana wa jimbo la California Gavin Newsom aliyempokea Trump jimboni mwake, amekiri kuwepo matatizo katika utunzaji wa misitu, na kusisitiza kuwa tatizo ni kubwa zaidi ya hapo. Maeneo makubwa ya misitu katika majimbo ya California, Oregon na Washington yameangamizwa na moto huo ambao pia umewauwa watu wasiopungua 35. Mpinzani wa Trump katika uchaguzi ujao, Joe Biden wa chama cha Democratic amemshutumu rais huyo kuwa mchocheaji wa mioto hiyo.,

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine amekanusha mchango wa mabadiliko ya tabia nchi katika ongezeko la mioto ya msituni inayoteketeza misitu magharibi mwa nchi yake, akisema bila kunukuu ushahidi wowote wa kisayansi kuwa viwango vya joto duniani vitaanza kushuka.

 Badala yake, Trump amesema tatizo kuhusiana na mioto hiyo sio mabadiliko ya tabianchi, bali ni utunzaji mbaya wa misitu. 

Gavana wa jimbo la California Gavin Newsom aliyempokea Trump jimboni mwake, amekiri kuwepo matatizo katika utunzaji wa misitu, na kusisitiza kuwa tatizo ni kubwa zaidi ya hapo. 

Maeneo makubwa ya misitu katika majimbo ya California, Oregon na Washington yameangamizwa na moto huo ambao pia umewauwa watu wasiopungua 35. 

Mpinzani wa Trump katika uchaguzi ujao, Joe Biden wa chama cha Democratic amemshutumu rais huyo kuwa mchocheaji wa mioto hiyo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *