Trump atuma ujumbe wa video akiwa hospitalini

October 4, 2020

Dakika 4 zilizopita

Donald Trump releases a video from his hospital room

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa yuko vizuri, lakini ndani ya siku chache zijazo zitakuwa za jaribio la kweli.

Ameweka video katika kurasa yake ya Twitter akiwa hospitalini, ambako anatibiwa Covid-19.

Daktari wake alisema jioni ya Jumamosi kuwa Bwana Trump anaendelea vizuri lakini bado anahitaji kuendelea na matibabu.

Trump amesema nini katika video yake kutoka hospitalini?

Ndani ya ujumbe wa dakika nne ambao bwana Trump, aliuweka mtandaoni akiwa amevaa koti bila tai, amewashukuru madaktari na wahudumu wa afya katika hospitali ya ‘Walter Reed National Military Medical Center’ iliyoko karibu na Washington DC, kituo cha afya ambacho anapata matibabu.

“Nilivyokuja hapa , nilikuwa sijisikii vizuri sana, lakini sasa najisikia nafuu, nnajisikia vizuri sana,” alisema, na kuongeza: “Baada ya siku chache zijazo nadhani nitakuwa na jaribio la kweli. Tutaona nini kitatokea baada ya hizo siku chache zijazo.”

Alisema anataka kurudi kwenye kampeni.

“Nadhani nitarudi kwenye kampeni punde tu. Ninaangalia namna ya kumaliza kampeni zangu jinsi nilivyoanza,” alisema.

“Tunaenda kuvitokomeza virusi hivi vya corona au vyovyote vile unavyotaka kuviita. Na tunaenda kuvishinda vizuri.”

Daktari wake binafsi Sean Conley alisema Jumamosi kwamba Trump hapokei matibabu ya oksijeni na pia ndani ya kipindi cha saa 24, homa imeonesha kuisha.

Daktari Conley aliashiria matumaini makubwa sana kwa afya ya rais lakini akaongeza kwamba hawezi kusema ni lini ataruhusiwa kutoka hospitali.

Rais huyo mwenye miaka 74, ambaye ni mwanaume na aliye kwenye kundi la wenye uzito kupita kiasi, ni miongoni mwa walio kwenye hatari ya maambukizi ya corona.

Hadi kufikia sasa amekuwa akipata matibabu ya sindanio na tiba ya kuzuia virusi ya remdesivir.

Mke wa rais Melania Trump, ambaye pia amethibitishwa kupata maambukizi ya Covid-19, pia nae “anaendelea vizuri”, amesema Daktari Conley.

1px transparent line

Orodha ya watu wengine ambao wamethibitishwa kupata maambukizi walio karibu na Bwana Trump ni pamoja na msaidizi wake Hope Hicks – anayeaminika kuwa wa kwanza kuonesha dalili – mkuu wa timu ya kampeni Bill Stepien na aliyekuwa mshauri wa Ikulu Kellyanne Conway. Maseneta wa Republican Mike Lee na Thom Tillis pia nao wamesemakana kupata maambukizi.

Awali, rais Donald Trump alipelekwa hospitali akiwa na homa baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Ikulu ya Marekani ilisema rais alikuwa mchovu lakini hali yake iko sawa na alipelekwa hospitali ya jeshi la taifa ya Walter Reed kama hatua ya kuchukua tahadhari.

Aidha, Trump alipelekwa hospitali chini ya saa 24 baada ya kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Vipi kuhusu hali ya kisiasa?

Kongozi mwenye ushawishi Republican Mitch McConnell alisema maseneta watahairisha kazi zake mpaka Oktoba 19, lakini kati inayohusisha tume ya majaji itaendelea – ambayo itaangalia uteuzi wa Jaji Barrett.

Trump atabaki kuwa na mamlaka.Makamu wa rais Mike Pence, mbaye chini ya katiba angepaswa majukumu ya rais amekutwa hana virusi vya corona.

Timu ya kampeni ya Trump ilisema Jumamosi kuwa itaendelea kwa kasi ileile mpaka rais arudi katika kampeni.

Joe Biden attends a virtual event in Wilmington, Delaware

Maelezo ya picha,

Joe Biden anaendelea na kampeni

Joe Biden anaendelea na kampeni ingawa ameliondoa tangazo ambalo lina muonekano hasi kuhusu rais.

Alisema katika safari yake ya Michigan : “Staki kumshambulia rais na mke wake kwa sasa.”

Lakini aliongeza kusema kuwa rais hakukabiliana na janga hili vizuri.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *