Trump atoka hospitalini

October 6, 2020

Trump alitoka kwenye hospitali ya Walter Reed iliyo mjini Bethesda, jimbo la Maryland mwendo wa saa kumi na mbili na dakika thelathini na tisa na kupelekwa kwa gari hadi kwenye helikopta ya kijeshi iliyokuwa imeegeshwa karibu na hospitali hiyo na kuondoka bila kuwahutubia waandishi wa habari.

Mapema Jumatatu, daktari wa rais huyo, Sean Conley, alisema kwamba ingawa hakuwa amepona kabisa, vipimo walivyovifanya vilionyesha kwamba ni sawa kwake kurejea kwenye ikulu.

“Ndani ya White House kuna wataalam wa afya wanaoweza kumwangalia saa 24 kwa siku,” alisema Dkt Conley.

Kila siku mgonjwa anapoendelea kukaa kwa hospitali bila haja ya kuwa mle, anahatarisha maisha yake. Kwa sasa hakuna husduma yoyote anayopata hapa hospitalini anmabayo hawezi kupata kwa ikulu,” aliongeza.

Kwa mujibu wa madaktari, Trump anendelea kutibiwa kwa dawa aina tatu ikiwemo ile ya Remdesivir, ambayo iko kwa awamu ya majaribio.

Iliripotiwa Ijumaa wiki iliyopita kwamba Trump na mkewe Melania Trump, walikuwa wameambukizwaa virusi vya corona, na baadaye siku hiyo, Rais huyo akapelekwa hospitalini.

Trump amekuwa miongoni mwa viongozi wa dunia walioambukizwa ugonjwa huo, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Honduras Juan Orlando Hernandez, Rais wa Bolivia Jeanine Anez na kiongozi wa Armenia Nikol Pashinyan.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *