Trump atetea wafuasi wake kuhusu makabiliano makali yaliyotokea Portland, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 6:00 am

September 1, 2020

 Rais wa Marekani Donald Trump ametetea wafuasi wake kwa madai ya mchango wao kwenye makabiliano yaliyotokea hivi karibuni.Amesema kwamba kijana anayeshutumiwa kwa mauaji ya watu wawili huko Wisconsin wiki iliyopita na wafuasi wa Trump walioshiriki makabiliano Oregon Jumamosi, walichukua hatua hiyo kujitetea.Bwana Trump aliongeza kwamba mpinzani mwenzake wa chama cha Democratic Joe Biden hajawapinga wanaharakati wa mrengo wa kushoto wanaoshutumiwa kwa kusababisha vurugu.Bwana Biden anaongoza kwenye kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Novemba.Jumatatu akiwa Ikulu ya Marekani wakati anafanya mkutano na wanahabari, Bwana Trump alimlaumu Bwana Biden na washirika wake kwa vurugu zilizotokea kwenye jimbo ambalo meya na gavana ni wa chama cha Democratic.Mwanahabari wa CNN alimuuliza rais ambaye anatoka chama cha Republican ikiwa atashutumu wafuasi wake ambao walifyatua risasi wakati wa makabiliano na waandamanaji wengine yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita Portland, Oregon.Wakati wa makabiliano hayo, mtu mmoja wa mrengo wa kulia Patriot Prayer, aliuawa na inasemekana mshukiwa amejieleza kuwa mfuasi wa kundi la antifa.Jumatatu, polisi walimtaja mwanaume aliyepigwa risasi kuwa ni Aoron Danielson. Kufikia sasa, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.”Naelewa kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao ni wafuasi, lakini hayo yalikuwa maandamano ya amani,” Bwana Trump alimjibu mwanahabari wa CNN, na yeye mwenyewe amekuwa akishutumu vyombo vya habari vya Marekani kwa kupuuza maandamano yanayotekelezwa na kundi la Black Lives Matter.”Rangi kama njia ya kujilinda rangi sio risasi.”Wafuasi wako na ni wafuasi wako kweli, walimpiga risasi mwanaume mmoja kijana na kumuua, sio kwa rangi lakini kwa risasi. Na nafikiria hilo ni jambo baya.”Mwanahabari mwingine alimuuliza Trump ikiwa atashutumu ufyatuaji wa risasi uliotokea Kenosha, Wisconsin, ambaye inasemekana aliwahi kuhudhuria moja ya mikutano ya rais.Kyle Rittenhouse, 17, anashutumiwa kwa mauaji ya watu watatu , Tukio hilo lililotokea wakati wa maandamano mjini humo yaliosababishwa na hatua ya Jacob Blake kupigwa risasi.”Yote hayo tunayafuatilia,” Bwana Trump amesema, “ni hali ambayo inazua maswali, mliona nilichokiona mimi, nafikiri alikuwa anajaribu kuondoka, inaonekana hivyo. Akaanguka na wakaanza kumshambulia.,

 

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea wafuasi wake kwa madai ya mchango wao kwenye makabiliano yaliyotokea hivi karibuni.

Amesema kwamba kijana anayeshutumiwa kwa mauaji ya watu wawili huko Wisconsin wiki iliyopita na wafuasi wa Trump walioshiriki makabiliano Oregon Jumamosi, walichukua hatua hiyo kujitetea.

Bwana Trump aliongeza kwamba mpinzani mwenzake wa chama cha Democratic Joe Biden hajawapinga wanaharakati wa mrengo wa kushoto wanaoshutumiwa kwa kusababisha vurugu.

Bwana Biden anaongoza kwenye kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Novemba.

Jumatatu akiwa Ikulu ya Marekani wakati anafanya mkutano na wanahabari, Bwana Trump alimlaumu Bwana Biden na washirika wake kwa vurugu zilizotokea kwenye jimbo ambalo meya na gavana ni wa chama cha Democratic.

Mwanahabari wa CNN alimuuliza rais ambaye anatoka chama cha Republican ikiwa atashutumu wafuasi wake ambao walifyatua risasi wakati wa makabiliano na waandamanaji wengine yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita Portland, Oregon.

Wakati wa makabiliano hayo, mtu mmoja wa mrengo wa kulia Patriot Prayer, aliuawa na inasemekana mshukiwa amejieleza kuwa mfuasi wa kundi la antifa.

Jumatatu, polisi walimtaja mwanaume aliyepigwa risasi kuwa ni Aoron Danielson. Kufikia sasa, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

“Naelewa kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao ni wafuasi, lakini hayo yalikuwa maandamano ya amani,” Bwana Trump alimjibu mwanahabari wa CNN, na yeye mwenyewe amekuwa akishutumu vyombo vya habari vya Marekani kwa kupuuza maandamano yanayotekelezwa na kundi la Black Lives Matter.

“Rangi kama njia ya kujilinda rangi sio risasi.

“Wafuasi wako na ni wafuasi wako kweli, walimpiga risasi mwanaume mmoja kijana na kumuua, sio kwa rangi lakini kwa risasi. Na nafikiria hilo ni jambo baya.”

Mwanahabari mwingine alimuuliza Trump ikiwa atashutumu ufyatuaji wa risasi uliotokea Kenosha, Wisconsin, ambaye inasemekana aliwahi kuhudhuria moja ya mikutano ya rais.

Kyle Rittenhouse, 17, anashutumiwa kwa mauaji ya watu watatu , Tukio hilo lililotokea wakati wa maandamano mjini humo yaliosababishwa na hatua ya Jacob Blake kupigwa risasi.

“Yote hayo tunayafuatilia,” Bwana Trump amesema, “ni hali ambayo inazua maswali, mliona nilichokiona mimi, nafikiri alikuwa anajaribu kuondoka, inaonekana hivyo. Akaanguka na wakaanza kumshambulia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *