Trump asema anaendelea vizuri hospitalini,

October 4, 2020

 

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa hospitalini tangu Ijumaa baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa COVID-19. 

Madaktari wake wameridhika na maendeleo ya matibabu yake. Waandishi habari ambao kwa kawaida huongozana na rais, hata hivyo, wamesema kwamba katika saa 24 zilizopita hali ya kiafya ya rais huyo ilikuwa ni ya wasiwasi wakinukuu chanzo cha kuaminika. 

Katika video inayomuonesha akiwa hospitalini, Trump amesema kwamba awali kweli alikuwa akijisikia vibaya wakati alipopelekwa hospitali, lakini sasa hivi anaendelea vizuri. 

Aidha rais huyo alitetea uamuzi wake wa kuendelea na mikutano yake ya kampeni ya watu wengi licha ya kitisho cha janga la virusi vya corona. 

Trump alisema hakuwa na jinsi, kama kiongozi alilazimika kukabiliana na changamoto hiyo kwani hakuwa tayari kujifungia ndani wakati wote.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *