Trump amshambulia Joe Biden, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 28, 2020

Rais Donald Trump amemshambulia Joe Biden kuwa ameingia katika siasa kwa bahati mbaya na kwamba atahatarisha usalama wa Marekani. Ameyasema hayo wakati akikubali uteuzi wa chama chake katika hotuba aliyoitoa akiwa katika Ikulu ya nchi hiyo ya White House jana.Wakati janga la virusi vya corona linawauwa Wamarekani 1,000 kila siku, Trump alikaidi miongozo ya utawala wake kupambana na janga hilo na kuzungumza kwa zaidi ya saa moja mbele ya kundi la watu waliokaa kwa kukaribiana, ambao kwa sehemu kubwa hawakuvaa barakoa.Akikabiliwa na hali ya mtafaruku wa ubaguzi, kuporomoka kwa uchumi na dharura ya kiafya ya taifa, Trump alitoa mtazamo wa ushindi na matumaini kwa hali ya baadae ya Marekani. Lakini alisema matumaini hayo yanaweza kupatikana iwapo atamshinda mgombea wa chama cha Democratic, ambaye kwa sasa anaongoza katika uchunguzi wa maoni katika majimbo muhimu na taifa kwa jumla.,

Rais Donald Trump amemshambulia Joe Biden kuwa ameingia katika siasa kwa bahati mbaya na kwamba atahatarisha usalama wa Marekani. 

Ameyasema hayo wakati akikubali uteuzi wa chama chake katika hotuba aliyoitoa akiwa katika Ikulu ya nchi hiyo ya White House jana.

Wakati janga la virusi vya corona linawauwa Wamarekani 1,000 kila siku, Trump alikaidi miongozo ya utawala wake kupambana na janga hilo na kuzungumza kwa zaidi ya saa moja mbele ya kundi la watu waliokaa kwa kukaribiana, ambao kwa sehemu kubwa hawakuvaa barakoa.Akikabiliwa na hali ya mtafaruku wa ubaguzi, kuporomoka kwa uchumi na dharura ya kiafya ya taifa, Trump alitoa mtazamo wa ushindi na matumaini kwa hali ya baadae ya Marekani. 

Lakini alisema matumaini hayo yanaweza kupatikana iwapo atamshinda mgombea wa chama cha Democratic, ambaye kwa sasa anaongoza katika uchunguzi wa maoni katika majimbo muhimu na taifa kwa jumla.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *