Trump amshambulia Joe Biden, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 3, 2020 at 1:00 pm

September 3, 2020

 Rais Donald Trump wa Marekani amehutubia katika tukio la kumbukumbu ya ushindi wa nchi hiyo katika vita vikuu vya pili vya dunia jana, akisifu nguvu za Marekani na pia akipenyeza matamshi ya kumsema hasimu wake katika kinyang’anyiro cha urais nchini humo Joe Biden. Trump alisimama mbele ya meli ya kivita ya enzi za vita vikuu vya pili vya dunia na kuutangaza mji wa bandari wa Wilmington, Carolina ya kaskazini, kuwa “mji wa turadhi.” Aliwapa tuzo za heshima maveterani wa vita, ikiwa ni pamoja na mwanajeshi wa zamani Hershel Woody Williams mwenye umri wa miaka 97, ambaye ni mwanajeshi pekee wa jeshi la majini la wakati wa vita ambaye yu hai bado na kumpa medali ya heshima. Mzaliwa huyo wa jimbo la Virginia alipigana katika vita vya Iwo Jima katika bahari ya Pasifiki. Trump alimshambulia Joe Biden kwa kusema anamfahamu mtu mwenye umri wa miaka 78 ambaye hayuko makini kama mzee huyo wa miaka 97.,

 

Rais Donald Trump wa Marekani amehutubia katika tukio la kumbukumbu ya ushindi wa nchi hiyo katika vita vikuu vya pili vya dunia jana, akisifu nguvu za Marekani na pia akipenyeza matamshi ya kumsema hasimu wake katika kinyang’anyiro cha urais nchini humo Joe Biden. 

Trump alisimama mbele ya meli ya kivita ya enzi za vita vikuu vya pili vya dunia na kuutangaza mji wa bandari wa Wilmington, Carolina ya kaskazini, kuwa “mji wa turadhi.” 

Aliwapa tuzo za heshima maveterani wa vita, ikiwa ni pamoja na mwanajeshi wa zamani Hershel Woody Williams mwenye umri wa miaka 97, ambaye ni mwanajeshi pekee wa jeshi la majini la wakati wa vita ambaye yu hai bado na kumpa medali ya heshima. 

Mzaliwa huyo wa jimbo la Virginia alipigana katika vita vya Iwo Jima katika bahari ya Pasifiki. Trump alimshambulia Joe Biden kwa kusema anamfahamu mtu mwenye umri wa miaka 78 ambaye hayuko makini kama mzee huyo wa miaka 97.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *