Trump aenda Kenosha, bila ya kukaribishwa, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 1:00 pm

September 1, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump anazipeleka leo kampeni zake za kutaka kuchaguliwa tena zenye kauli mbiu ya utiifu wa sheria katika eneo lenye mivutano la Kenosha ambako kumetokea tukio la karibuni kabisa la polisi kumfyatulia risasi Mmarekani mweusi akipuuza onyo kuwa hakaribishwi mjini humo. Wakati akizuru jimbo muhimu la uchaguzi la Wisconsin Trump amesema hana mipango ya kukutana au kuzungumza na familia ya Jacob Blake, aliyepigwa risasi mgongoni mara kadhaa huku watoto wake watatu wakitazama wakiwa kwenye gari. Badala yake Trump atashauriana na polisi na kujionea uharibifu uliotokana na machafuko yaliyozuka mjini humo baada ya Blake kupigwa risasi na polisi mzungu mnamo Agosti 23. Tukio hilo lilimfanya Blake kupooza kuanzia kiunoni hadi miguuni.,

Rais wa Marekani Donald Trump anazipeleka leo kampeni zake za kutaka kuchaguliwa tena zenye kauli mbiu ya utiifu wa sheria katika eneo lenye mivutano la Kenosha ambako kumetokea tukio la karibuni kabisa la polisi kumfyatulia risasi Mmarekani mweusi akipuuza onyo kuwa hakaribishwi mjini humo. 

Wakati akizuru jimbo muhimu la uchaguzi la Wisconsin Trump amesema hana mipango ya kukutana au kuzungumza na familia ya Jacob Blake, aliyepigwa risasi mgongoni mara kadhaa huku watoto wake watatu wakitazama wakiwa kwenye gari. 

Badala yake Trump atashauriana na polisi na kujionea uharibifu uliotokana na machafuko yaliyozuka mjini humo baada ya Blake kupigwa risasi na polisi mzungu mnamo Agosti 23. Tukio hilo lilimfanya Blake kupooza kuanzia kiunoni hadi miguuni.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *