Tofauti za kisiasa zatishia kusambaratisha serikali za kaunti Kenya

September 16, 2020

Dakika 5 zilizopita

Wycliff Oparanya

Baraza la magavana nchini Kenya (CoG) limeagiza serikali zote za kaunti kuwapeleka wafanyakazi wao kwa likizo ya wiki mbili mbali na kuahirisha huduma zote zisizo na umuhimu mkubwa kufuatia mkwamo wa fedha za kuendesha serikali hizo.

Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa mabaraza hayo na gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliff Oparanya amesema kwamba kufuatia mkutano wa baraza hilo uliofanyika tarehe 8 mwezi Septemba 2020, waliamua kwamba wafanyakazi wote walio katika sekta zisizo muhimu za kaunti watalazimika kwenda likizo .

Aidha Baraza hilo limesema kwamba vifaa vyote vya huduma za afya katika kaunti hizo havitaruhusu wagonjwa wapya kulazwa huku vikitoa huduma chache kwa wagonjwa wanaotibiwa na kwenda nyumbani.

Taarifa hiyo imesema kwamba tatizo la fedha kuendesha serikali hizo za kaunti linatokana na mkwamo uliopo katika bunge la seneti kuhusu kiwango cha fedha zinazopaswa kutolewakwa kila kaunti.

”Haijulikani ni lini mgogoro huo utatatuliwa hivyobasi tumelazimika kutoka notisi kwa kaunti zote kama ilivyo”, alisema Oparanya.

Magavana Kenya

Serikali za kaunti nchini Kenya zimeendelea kuendeshwa bila fedha zozote kwa miezi kadhaa sasa vaada ya bunge la seneti kufeli kukubaliana kuhusu mbinu itakayotumiwa na serikali ya kugawanya fedha katika kaunti hizo.

Serikali za kaunti zimesalia bila fedha kwa miezi kadhaa baada ya bunge la seneti kufeli kukubaliana kuhusu mbinu itakayotumika na serikali kugawanya fedha kwa serikali za kaunti. Kwa zaidi ya vikao kumi, bunge la seneti lilishindwa kupata njia itakayotumika, hatua iliopelekea kubuniwa kwa kamati ya watu 12 ambayo pia nayo iilfeli kupata suluhu jinsi dola bilioni 3.16 zitaganywa kwa serikali hizo za kaunti. Wafanyakazi katika kaunti wamefanya kazi bila mishahara kwa miezi kadhaa , ikiwemo wafanyakazi wa afya wakati muhimu wa mlipuko wa Covid 19. Mjadala katika bunge hilo la seneti nchini Kenya kuhusu ugavi wa fedha hizo miongoni mwa serikali za kaunti 47 una pande mbili ambazo zimeshindwa kuafikiana. Pande moja inadai kwamba idadi ya watu inafaa kutumiwa katika ugavi huo. Kundi jingine linapendekeza kwamba ukubwa wa ardhi unapaswa kuwa chanzo cha ugavi wa fedha hizo. Mbinu inayoyependekezwa na Tume ya ugavi wa mapato CRA inatokana na idadi ya watu.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akiunga mkono mpango huo, amehoji kwamba idadi ya watu ina athari kwa huduma kama vile Afya, elimu na miundo msingi.Pande hizo mbili zinasema kwamba mbinu ya kutumia idadi ya watu inazibagua kaunti za walio wachache ambazo zinaishi wafugaji. Zinasema kwamba ubaguzi huo sio ajali bali kitengo cha maendeleo ambacho kinapigania maendeleo ya haraka katika maeneo tofauti ambayo yanaonekana kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi ikilinganishwa na maeneo mengine. Maono yote mawili ni muhimu na hiyo ndio sababu Raila Odinga, huku akiunga mkono sera ya idadi ya watu pia anasema kwamba hoja zinazotolewa na wanachama wa jamii za wafugaji zinafaa kutiliwa maanani katika ugavi wa mapato katika siku zijazo. Kwa sasa ili kuzuia kusamabaratisha serikali za kaunti, kunapaswa kuwa na muafaka.

Source link

,Dakika 5 zilizopita Chanzo cha picha, TWITTER Baraza la magavana nchini Kenya (CoG) limeagiza serikali zote za kaunti kuwapeleka wafanyakazi…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *