Tiwa Savage afunguka alivyotaka kuacha muziki, on September 11, 2020 at 8:00 am

September 11, 2020

 Ugumu humkuta yeyote. Hii inathibitishwa na nyota wa muziki toka Nigeria Tiwatope Savage maarufu Tiwa Savage (40) baada ya kusimulia jinsi alivyokata tamaa na kutaka kuacha muziki.Kwenye mahojiano aliyofanya na Jarida la #NewYorkTimes, nyota huyo wa Nigeria alisema kuwa mwaka 2010 alikuwa karibu kuacha muziki baada ya kutoa wimbo wake “Love Me, Love Me, Love Me.”Wimbo huo ulifungiwa na shirika la habari Nigeria (NAN) kitu kilichopelekea hata baadhi ya matamasha yake kuahirishwa na kufanya msanii huyo akate tamaa kabisa na masuala ya muziki.Akielezea sababu iliyomsukuma kurudi kwenye biashara ya muziki alisema, “Baada ya kufanya maamuzi ya kuacha, kulikuwa na wasichana wengi waliokuwa wakinitumia ujumbe mara nimependa hereni zako, au mara nimependa ‘tattoo’ yako na hapo ndipo niliposema acha nirudi kwa ajili ya wasichana hawa.”“Mpaka sasa ninawahamasisha wasichana wengi lakini wao ndio walionihamasisha kurudi kwenye muziki,” alisema Tiwas Savage,

 

Ugumu humkuta yeyote. Hii inathibitishwa na nyota wa muziki toka Nigeria Tiwatope Savage maarufu Tiwa Savage (40) baada ya kusimulia jinsi alivyokata tamaa na kutaka kuacha muziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jarida la #NewYorkTimes, nyota huyo wa Nigeria alisema kuwa mwaka 2010 alikuwa karibu kuacha muziki baada ya kutoa wimbo wake “Love Me, Love Me, Love Me.”

Wimbo huo ulifungiwa na shirika la habari Nigeria (NAN) kitu kilichopelekea hata baadhi ya matamasha yake kuahirishwa na kufanya msanii huyo akate tamaa kabisa na masuala ya muziki.

Akielezea sababu iliyomsukuma kurudi kwenye biashara ya muziki alisema, “Baada ya kufanya maamuzi ya kuacha, kulikuwa na wasichana wengi waliokuwa wakinitumia ujumbe mara nimependa hereni zako, au mara nimependa ‘tattoo’ yako na hapo ndipo niliposema acha nirudi kwa ajili ya wasichana hawa.”

“Mpaka sasa ninawahamasisha wasichana wengi lakini wao ndio walionihamasisha kurudi kwenye muziki,” alisema Tiwas Savage

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *