Thiago Silva amejiunga na Chelsea akitokea PSG, noreply@blogger.com (Udaku Special)

August 28, 2020

Klabu ya Chelsea ya England imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Brazil Thiago Silva akiwa mchezaji huru baada ya mchezaji huyo kumalizika mkataba na klabu ya PSG ya Ufaransa na amesini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia The Blues.Thiago Silva anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Chelsea katika dirisha hili la majira ya kiangazi ambalo bado lipo wazi, wachezaji wengine ambao wamesajiliwa na Chelsea mpaka sasa ni Timo Werner, Hakim Ziyech, Xavier Mbuyamba, Ben Chilwell na Malang SarrSilva alijiunga na PSG mwaka 2012 akitokea AC Milan ya Italia, hivyo amewatumikia matajiri hao wa jiji la Paris kwa miaka nane ameshinda jumla ya mataji 23 katika kipindi hicho yakiwemo mataji 10 ya ligi kuu Ufaransa Ligue 1.Chelsea inaendelea kuboresha zaidi kikosi chao chini ya kocha Frank Lampard baada ya kufungiwa kutosajili msimu uliopita na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA baada ya kukiuka kanunu na taraibu za usajili.Pia The Blues wanaweza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa ujerumani anayecheza katika klabu ya Bayer Leverkusen Kai Havertz,

Klabu ya Chelsea ya England imekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Brazil Thiago Silva akiwa mchezaji huru baada ya mchezaji huyo kumalizika mkataba na klabu ya PSG ya Ufaransa na amesini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia The Blues.

Thiago Silva anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Chelsea katika dirisha hili la majira ya kiangazi ambalo bado lipo wazi, wachezaji wengine ambao wamesajiliwa na Chelsea mpaka sasa ni Timo Werner, Hakim Ziyech, Xavier Mbuyamba, Ben Chilwell na Malang Sarr

Silva alijiunga na PSG mwaka 2012 akitokea AC Milan ya Italia, hivyo amewatumikia matajiri hao wa jiji la Paris kwa miaka nane ameshinda jumla ya mataji 23 katika kipindi hicho yakiwemo mataji 10 ya ligi kuu Ufaransa Ligue 1.

Chelsea inaendelea kuboresha zaidi kikosi chao chini ya kocha Frank Lampard baada ya kufungiwa kutosajili msimu uliopita na shirikisho la soka ulimwenguni FIFA baada ya kukiuka kanunu na taraibu za usajili.

Pia The Blues wanaweza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa ujerumani anayecheza katika klabu ya Bayer Leverkusen Kai Havertz

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *