Tetesi za soka Ulaya Jumanne 15.09.2020: Bale, Alcantara, Origi, Messi, Sancho, Torreira, Suarez, Koulibaly

September 15, 2020

Dakika 2 zilizopita

Liverpool itasubiri mpaka wiki ya mwisho ya dirisha la usajili ili kumsajili rasmi kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara

Liverpool itasubiri mpaka wiki ya mwisho ya dirisha la usajili ili kumsajili rasmi kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara,29. (Talksport)

Manchester United ipo tayari kumpa mkataba winga wa Madrid Gareth Bale ,31 kukaa kwa mkopo klabuni hapo kwa makubaliano ya kupewa mkataba baada ya kuonekana kumkosa winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho ,20. (Sun)

Lakini mshambuliaji huyo wa Wales hataki uhamisho wa mkopo. (Mail)

Manchester United ipo tayari kumpa mkataba winga wa Madrid Gareth Bale

Manchester United inahofia kuongezeka kwa ushindani katika kumnasa Sancho msimu ujao ikiwa hawatamchukua katika msimu huu wa dirisha la usajili. (ESPN)

Mchezaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, ataombwa na rais wa klabu Josep Maria Bartomeu kukatwa mshahara. (Deportes Cuatro – in Spanish)

Manchester City imetoa ofa ya pauni milioni 82 na pauni milioni 4.5 kwa ajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Atletico Madrid Jose Gimenez, 25. (AS – in Spanish)

Lionel Messi, ataombwa na rais wa klabu Josep Maria Bartomeu kukatwa mshahara

Klabu ya Fenerbahce iko kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu kumsajili mshambuliaji Divock Origi, huku Aston Villa, Newcastle, Brighton na Fullham zikimtaka mchezaji huyo, 25. (Mirror)

Araenal inaweza kumruhusu Lucas Torreira, 24, kuondoka kwa mkopo kabla ya msimu wa dirisha la usajili kumalizikka, huku Fiorentina na Torino wakiwa wanamtaka kiungo huyo wa kati. (Guardian)

Kama Manchester City au Paris St-Germain hawatamaliza mchakato wa kumnyakua Msenegali Kalidou Koulibaly mpaka mwishoni mwa juma, Napoli wanatarajiwa kumtoa sokoni mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi, 29. (Football Italia)

Aston Villa, Newcastle, Brighton na Fullham zinamtaka Divock Origi

Manchester United wako kwenye mazungumzo na Real Madrid kwa ajili ya Mhispania Sergio Reguilon. (Marca)

Klabu ya Sevilla, ambayo Reguilon ameutumia msimu uliopita akicheza kwa mkopo, imemsajili beki wa kushoto wa Sporting Marcos Acuna, 28. (Evening Standard)

West Ham wanajaribu kumnasa mlinzi wa Uingereza James Tarkowski ,27, baada ya Burnley kukataa ofa ya awali ya £30m. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez anatarajiwa kumaliza msimu wake akiwa benchi wakati mkataba wake ukikaribia kumalizika. Suarez mwenye miaka 33 raia wa Uruguay ameambiwa atafute klabu mpya huku akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.(ESPN)

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez anatarajiwa kumaliza msimu wake akiwa benchi

Kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher, 20, atajiunga na West Bromwich Albion kwa mkopo na anajiandaa kusaini mkataba mpya Stamford Bridge .(Football.London)

Mlinda mlango Emi Martinez, 28, anakamilisha mpango wa uhamisho wa thamani ya pauni milioni 20 kwenda Aston Villa baada ya kuchagua kuondoka kwa washika bunduki. (Evening Standard)

Aston Villa iko mbioni kukamilisha mpango wa kumnasa mshambuliaji Bertrand Traore ,25, kutoka Lyon. (Telegraph, subscription required)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Msenegali Kalidou Koulibaly

Tottenham wanapenda kumsajili mshambuliaji wa Norway Alexander Sorloth, 24, kwa mujibu wa rais wa Trabzonspor Ahmet Agoglu. Sorloth kwa sasa anacheza kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Uturuki akitokea Crystal Palace. (Independent)

Maafisa wa Werder Bremen wamethibitisha kuwa walifuatwa na Aston Villa kwa ajili ya kiungo wa kati Milot Rashica, 24. (Deichstube, via Birmingham Mail)

Aston Villa imepatia mshambuliaji Keinan Davis, 22, mkataba wa miaka mitatu. (Football Insider)

Source link

,Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Liverpool itasubiri mpaka wiki ya mwisho ya dirisha la usajili ili kumsajili rasmi…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *