Tetesi za soka Ulaya Jumanne 06.10.2020: Pochettino, Garcia, Shaqiri, Stones, Anderson, Dawson

October 6, 2020

Dakika 3 zilizopita

Mauricio Pochettino

Maafisa wakuu wa klabu ya Manchester United wamewasiliana na aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino iwapo watamfuta meneja Ole Gunnar Solskjaer. (Star)

Manchester City imekataa ofa ya dau la £15.4m na marupurupu kutoka kwa klabu ya Barcelona kumnunua beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.. (Sky Sports)

Liverpool ilipokea maombi ya winga wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 28, wakati wa dirisha la uhamisho na wanataraji atasalia katika klabu hiyo hadi mwezi Januari kwasasabu hawako tayari kumuuza kwa mkopo (Goal)

Xhedan Shakiri

Beki wa Manchester City na England John Stones, 26, alikataa mbadala wa kuondoka kwa mkopo kuelekea Totenham kwasababu hakutaka kuiondoa familia yake. (Star)

Klabu ya Porto ina hamu ya kumnunua mchezaji wa West Ham na Brazil Felipe Anderson, 27, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Sky Sports)

West Ham iko katika mazungumzo ya kumsajili beki wa England mwenye umri wa miaka 30 Craig Dawson kutoka Watford. (Football Insider)

Barcelona imepoteza zaidi ya £181m kama mapato kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. (Telegraph)

Felipe Anderson

Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel hafurahii hatua ya klabu hiyo kushindwa kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho. (Guardian)

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *