Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 19.09.2020: Bale, Dembele, Mendy, Telles,Traore, Brewster

September 19, 2020

Dakika 4 zilizopita

Gareth Bale

Baadhi ya wachezaji wa Real Madrid wanadai kuridhishwa na hatua ya kuondoka kwa mshambuliaji wa wa kimataifa wa Wales Gareth Bale kuhamia Tottenham kwa mkopo. (AS – in Spanish)

Rennes wanataka Chelsea kuwajumuisha wachezaji wawili katika mkataba wowowte utakaowahusisha kipa wa kimataifa wa Senegal Edouard Mendy, 28. Beki wa England Fikayo Tomori, 22, ni mmoja wa wachezaji wanaotakiwa na klabu hiyo ya Ufaransa. (Football Insider)

Liverpool imeulizia uwezekano wa kumpata kwa mkopo winga wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele, 23. (Sport)

Ousmane Dembele

Maelezo ya picha,

Winga wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele

Manchester United wameafikiana na Porto kumhusu beki wao Alex Telles and the 27- sasa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil anaweza kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo. (RMC Sport – via Mirror)

United sasa wanahitaji kufany ahima kukamilisha mchakato wa usajili ili kumpata nyota huyo baada ya Paris St-Germain kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsaka Telles. (O Jogo – in Portuguese)

Nicolas Otamendi

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Nicolas Otamendi, 32, kuhamia City

Manchester City wanapania kumsajili beki wa kati na nyuma wa Sevilla Jules Kounde, 21.Hatua hiyo huenda ikamfanya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Nicolas Otamendi, 32, kuhamia City. (Telegraph)

Mkufunzi wa Sheffield United Chris Wilder amesema klabu hiyo imefanya mazungumzo na Liverpool kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Muingereza Rhian Brewster, 20 kwa mkopo. (Yorkshire Live)

Rhian Brewster

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji Muingereza Rhian Brewster anayesakwa na Crystal Palace

Lakini Crystal Palace pia wanataka kumsajili Brewster kutoka kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya England kwa mkataba wa kudumu. (90Min)

Source link

,Dakika 4 zilizopita Chanzo cha picha, EPA Baadhi ya wachezaji wa Real Madrid wanadai kuridhishwa na hatua ya kuondoka kwa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *