Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 10.10.2020:Messi, Haaland, Sancho, Pogba, De Bruyne, Saliba

October 10, 2020

Dakika 3 zilizopita

Messi

Manchester City itaweza kumsajili kiungo mchezeshaji kutoka Barcelona, Muargentina Lionel Messi, 33, msimu ujao kama fursa hiyo itajitokeza, anasema Afisa mkuu uendeshaji Omar Berrada. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, raia wa Norway striker Erling Haaland, 20, na winga wa klabu hiyo, kutoka England Jadon Sancho, 20, bado wako kwenye orodha kuu ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya Manchester United. (ESPN)

Real Madrid imeoondoa uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, baada ya kusema ilikuwa ndoto yake kuchezea klabu hiyo siku moja. (AS – in Spanish)

Kelvin

Kiungo wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 29, anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka miwili wenye thamani ya £300,000 kwa wiki kusalia Manchester City. (Sun)

Beki wa Arsenal’s aliyesajiliwa kwa £27m Mfaransa William Saliba, ambaye hajacheza mchezo wowote wa ligi msimu huu, anajiandaa kucheza Championship kwa mkopo, Brentford ikionyesha nia ya kumtaka kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. (Goal)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, anajiandaa kucheza mchezo wake wa kwanza wakati huu akirejea kuichezea Tottenham kwa mara ya pili dhidi ya West Ham mwishoni mwa wiki ijayo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34, anasema alikaribia kutua ligi ya Serie A, wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari na dirisha kubwa lililofungwa wiki iliyopita. (RMC Sport, via Football London)

Aston Villa wanapanga kupunguza gharama za mishahara kwa kuuza baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho, wakijiandaa kumsainisha mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28, ambaye anawaniwa pia na West Ham. (Football Insider)

Frederic Guilbert

Villa inajiandaa kuwauza winga wake mdachi Anwar El Ghazi, 25, beki mfaransa Frederic Guilbert, 25, na kiungo wa Muingerereza, Henri Lansbury, 29, kabla dirisha la usajili wa ndani kufungwa Oktoba 16. (Football Insider)

Manchester City wana matumaini Pep Guardiola atasaini mkataba mpya, lakini watatafuta mrithi wake iwapo meneja huyo ataonyesha dalili za kutaka kuondoka. (Telegraph)

Kiungo wa Hispania Dani Ceballos, 24, anasema alikuwa na shauku ya kurejea kwa mkopo Arsenal licha ya Real Madrid kumtaka kusubiri kwa mwezi mmoja. (Marca)

Kiungo wa Kiingereza Jack Wilshere, 28, anataka kuchezea klabu ya La Liga au Serie A baada ya kutemwa na West Ham. (Talksport)

Winga wa Kifaransa Allan Saint-Maximin, 23, anasema atakuwa na furaha kusalia Newcastle kwa muda mrefu- kama Magpies watafuata matamanio aliyonayo. (Newcastle Chronicle)

beki wa Senegal Kalidou Koulibal
Maelezo ya picha,

Beki wa Senegal Kalidou Koulibal

Manchester City hawakuweka nguvu kubwa kumsajili beki wa Senegal Kalidou Koulibaly, 29, kutoka Napoli. (The Athletic, via Inside Futbol)

Beki wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka, 22, ameondoa bendera ya England katika Ukurasa wake wa Instagram na kuweka bendera ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Beki huyo wa kulia, mzaliwa wa Croydon anaruhusiwa kuchezea mataifa hayo mawili kwenye timu za wakubwa, akiwa amezichezea timu za vijana za mataifa hayo. (Goal)

Mshambuliaji wa Leicester, kutoka Algerian Islam Slimani, 32, ambaye amecheza kwa mkopo misimu miwili iliyopita akikaribia kuikacha klabuni hiyo, amegusia kwamba, huenda akawa kwenye mipango ya msimu huu ya kocha Brendan Rodgers. (Leicester Mercury)

Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen

Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, 28, na kiungo wa zamani wa Tottenham anasema anajisikia vibaya kuanza msimu huu akianzia benchi zaidi kwenye kikosi cha Inter Milan. (Independent)

Tottenham walikuwa na mipango ya ulioidhinishwa wa kujenga uwanja wa michezo kwenye eneo la mazoezi la timu hiyo huko Enfield ambalo limebuniwa kutumika kwa pamoja na kikosi cha kwanza na timu za vijana. (Football London)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametoa salamu za pongezi wa kwa John Lennon ambaye nyota huyo wa The Beatles angekuwa akisheherea miaka 80 ya kuzaliwa kwa kuimba nyimbo kadhaa za mtunzi huyo mashuhuri wa nyimbo. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Denmark Nicklas Bendtner amekiri kupenda sana mitindo ya maisha kutokana na pesa alizovuna kwa kuwa mchezaji wa kilpwa. (Guardian)

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *