Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 03.10.2020: Hudson-Odoi, Dembele, Sancho, Skriniar

October 3, 2020

Dakika 1 iliyopita

Callum Hudson-Odoi

Maelezo ya picha,

Callum Hudson-Odoi (kulia)

Bayern Munich inafanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kumchukua winga wa England Callum Hudson-Odoi kwa mkopo. (Sport Bild, via Mail)

Chelsea imeiarifu Inter Milan ingependelea kumuona beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso akiondoka kwa makubaliano ya kudumu baada ya upande wa Serie A kuonesha nia ya kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo, 29 kukiwa na chaguo la kumnunua kabisa. (Goal)

Leeds United imeanzisha tena nia yake ya kumsajili James kwa kutoa ofa ya pauni milioni 25 kwa Manchester United. (Football Insider)

Ousmane Dembele

Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, amebadili nia juu ya kujiunga na Manchester United – lakini klabu yake Barcelona haijathibitisha hatua yoyote ya uhamisho. (L’Equipe via Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 27, amemtaka mchezaji mwenzake wa Ufaransa Dembele kuhamia Old Trafford. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anajitayarisha kumuuza winga Daniel James, 22, kusaidia kupatikana kwa pesa za kumnunua winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20. Hata hivyo, Solskjaer bado hajafanikiwa kushawishi wakuu wa klabu hiyo kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales. (ESPN)

Reiss Nelson

Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema hajakuwa na mazungumzo yoyote kumhusu mshambuliaji wa Arsenal Reiss Nelson, 20, licha ya kuhusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo. (Mirror).

Diogo Dalot, 21, wa Manchester United anafanya mazungumzo na AC Milan – lakini Roma pia inataka kumsajili beki huyo wa kulia kuwa sehemu ya makubaliano yao kwa beki wa kati wa Uingereza Chris Smalling, 30. (Sun)

Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Uruguay Lucas Torreira, 24, amewasili Uhispania kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Atletico Madrid Jumamosi kabla ya kutimiza makubaliano ya mkopo ya muda mrefu kukiwa na chaguo la kumnunua kwa pauni milioni 18.1. (AS – in Spanish)

Milan Skriniar

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa Inter Milan, Milan Skriniar

Tottenham itafanya majaribio mapya ya kumsajili beki wa kati wa Inter na Slovakia Milan Skriniar, 25, wikendi hii baada ya mshambuliaji Carlos Vinicius wa Benfica kukamilisha mkataba wake wa mkopo. (Standard)

Tottenham pia imeulizia juu ya upatikanaji wa mchezaji wa kati wa Uturuki Merih Demiral, lakini Juventus haiko tayari kumuachilia mchezaji huyo, 22 kuondoka. (Goal)

Hatua ya Burnley ya kumnyatia winga wa Wales Harry Wilson, 23, huenda ikadidimia kwasababu haiko tayari kutoa kiwango cha pesa kinachohitajika cha pauni milioni 15 kwa Liverpool. (Football Insider)

Cameron Carter-Vickers

Maelezo ya picha,

Cameron Carter-Vickers mchezaji wa Tottenham

Bournemouth, Swansea City na Luton Town wa Ligi ya Mabingwa wote wanamnyatia mlinzi wa Tottenham na Marekani Cameron Carter-Vickers, 22. (Mail)

Arsenal iko tayari kumtoa beki wa kati William Saliba, 19, kwa mkopo huku mazungumzo na Rennes yakiwa yameshafanyika. (Guardian)

Inter Milan inakaribia kumsajili beki wa Parma na Italia Matteo Darmian, 30, katika makubaliano ya pauni milioni 1.81. (Goal)

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *