Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 11.09.2020: Aubameyang, Kante, Smalling, Wijnaldum, Rose, Ivanovic

September 11, 2020

Dakika 2 zilizopita

Pierre-Emerick Aubameyang, 31

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo. (Athletic – subscription required)

Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta, 27, ataweza kuondoka Aston Villa miezi minane tu baada ya kujiunga na klabu hiyo. (Mail)

Chelsea imekataa ofa ya Inter Milan kwa ajili ya kiungo wake aliyetwaa kombe la dunia N’Golo Kante, 29, ofa ambayo inajumuisha kubadilishana na kiungo wa Croatia Marcelo Brozovic, 27. (Guardian)

Mlinzi wa Manchester United Muingereza Chris Smalling, 30, hajahudhuria mazoezi wiki hii akikaribia kutua ligi ya Italia, Serie A, kwenye timu ya Roma, kwa uhamisho wa kudumu, timu ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita.(Telegraph – subscription required)

Kiungo wa Liverpool Georginio Wijnaldum, 29, amefanya mazungumzo yaliyoenda vizuri na meneja Jurgen Klopp kuhusu mustakabali wake klabuni hapo. Mholanzi huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake ya sasa pale Anfield. (Sky Sports)

Beki wa England na Tottenham Rose, 30, anakaribia kutimka ligi kuu ya Uingereza kujiunga na kikosi cha Serie A Genoa.(PA, via Team Talk)

Kipa wa Arsenal Muargentina Emiliano Martinez, 28, amekubali kandarasi ya miaka mine na Aston Villa, yenye thamani ya £60,000 kwa wiki, wakati huo vilabu hivyo vikitarajiwa kukubaliana ada ya uhamisho ya zaidi ya £15m. (Independent)

Kiungo wa Manchester United na Brazil Fred, 27, amepuuza ripoti kwamba anaweza kuondoka msimu huu na kujiunga Galatasaray na Uturuki. (Four Four Two)

West Brom wako kwenye mazungumzo ya kumnasa mlinzi wa zamani wa Chelsea Branislav Ivanovic, 36, kwa uhamisho huru baada ya kutemwa na Zenit St Petersburg ya Urusi.(Telegraph – subscription required)

Kiungo wa zamani wa Manchester United Ravel Morrison, 27, yuko kwenye mazungumzo na klabu za Uholanzi za Vitesse Arnhem na Utrecht baada ya kutemwa na Sheffield United. (Mail)

Mshambuliaji wa Liverpool na Wales Ben Woodburn, 20, anatarajiwa kujiunga na Sparta Rotterdam Uholanzi kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu mzima. (Standard)

Ofa ya Newcastle ya £32m imekataliwa na Lille kwa ajili ya kumsaini kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, Boubakary Soumare. (Fabrizio Romano)

Fulham inataka kumsajili kiungo wa kireno, kutoka Benfica, Florentino Luis, 21, kwa mkopo wa muda mrefu kwa sharti la kumsajili moja kwa moja kwa ada ya £27m. (Sun)

Porto imekataa ofa ya £22m kutoka Wolves kwa ajili ya kiungo wake Jesus Corona. Mkata wa nyota huyo wa Mexico mwenye miaka 27 una kipengele kinachotaka mpaka ilipwe ada ya £27m ndiyo aweze kuhama. (Mail)

Source link

,Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31 Mshambuliaji…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *