Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 08.10.2020: Dembele, Sarr, Rose, Anderson, Romero, Knockaert

October 8, 2020

Dakika 1 iliyopita

Ousmane Dembele
Maelezo ya picha,

Sijawahi kuwa na hamu ya kujiunga na man United

Mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele 23 hakuwa na hamu ya kujiunga na Manchester United kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho na sasa anataka kujiunga na Juventus msimu ujao.(Catalunya Radio, via Mirror)

Manchester United haitawasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Senegal na Watfotd Ismaila Sarr, 22, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho la ligi ya EFL tarehe 16. (Goal)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anatarajiwa kumwacha nje beki wa kushoto wa England Danny Rose, 30, katika kikosi chake cha wachezaji 25 ambacho kinatarajiwa kukamilika kufikia tarehe 20 Oktoba. (Mail)

Mchezaji wa Westaham na Brazil Felipe Anderson anasema anaafikia ndoto yake ya kushiriki katika mechi za ligi ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuhamia katika klabu ya Porto kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia , lakini anaamini kwamba bado ataendelea kuichezea West (Talksport)

West Ham ina hamu ya kuongezea beki wa kati kutoka ligi ya daraja la kwanza nchini England huku pia wakitafuta kiungo wa kati atakayeziba pengo lililowachwa na Anderson . (London Evening Standard)

Kipa wa Manchester United na Argentina Sergio Romero, 33, anajiandaa kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS baada ya kukosa kujiunga na klabu ya Everton katika siku ya mwisho ya dirisha la. (Mail)

Mkufunzi mpya wa Nottingham Forest Chris Hughton anafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Fulham na Ufaransa Anthony Knockaert, 28, on loan. (Sky Sports)

West Brom wana imani ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Huddersfield na Karlan Grant, 23, kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika ligi ya EFL Ijumaa ijayo. (Mail)

MKufunzi wa Ujerumani Joachim Low andai kwamba beki wa Clsea na Ujerumani Antonio Rudiger “alijatribu kufanya kila kitu kuondoka Chelsea kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho na anaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atawasilisha ombi la kutaka kuondoka katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Sun)

Bayern Munich, ambao walishindwa kuafikiana kuhusu mkataba wa kumsajili kwa mkopo winga wa England Callum Hudson Odoi 19 waliambiwa na Chelsea kwamba watapewa adhabu iwapo mchezaji huyo hatashirikishwa katika mechi nyingi katika ligi ya Bundesliga mbali na kifungu cha sheria cha Bayern lumnunua kwa zaidi ya £70m iwapo atacheza idadi fulani ya mechi. (Sport Bild)

KIungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 25, amefichua kampeni yake ya wiki tatu kumshawishi kiungo wa kati wa England kujiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea. (London Evening Standard)

Grealish alikuwa mmoja wa wachezaji wanne waliokuwa wakilengwa na mkufunzi wa Man United Solskjaer ambaye alishindwa kuwasaini kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (ESPN)

Mshambuliaji mpya wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 33, amefichua kwamba anataka kuichezea klabu ya Boca Juniors baada ya kuondoka katika uwnaja wa Old Trafford.. (Goal)

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *