Tetesi za soka kimataifa, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 6:00 am

September 1, 2020

 Lionel Messi ataondoka Barcelona msimu hii na ” inawezekana” akaelekea Manchester City, kwa mujibu wa mgombea wa urais wa klabu hiyo, Toni Freixa. (Goal)Barcelona inaamini kwamba njia pekee ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 33, kuondoka kihalali bure ni ikiwa ataahidi kwamba hatashiriki katika michuano ya msimu ujao.(ESPN)Rais wa Argentina, Alberto Fernandez, amemshauri Messi kurejea katika klabu yake ya ujana ya Newell’s Old Boys. (C5N, via Evening Standard)Chelsea imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, kwa kima cha kwanza cha pauni milioni 72, na kusababisha pesa za matumizi yao kipindi cha uhamisho kuongezeka hadi pauni milioni 200. (Guardian)Manchester United inamlenga mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 21. (ESPN)Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 24, anasemekana kwamba wiki hii atajiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Guardian)Vilabu vya Saudi Arabia na Qatar vimeonesha nia ya kumsajili Mjerumani Mesut Ozil msimu huu lakini mchezaji huyo wa Arsenal, 31, hana nia ya kuondoka London. (Telegraph)Tottenham imeanzisha mazungumzo ya mkataba mpya wa mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris, 33, licha ya kumsajili Joe Hart kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)Spurs inafanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Joshua King na pia inamnyatia mshambuliaji Mwingereza wa Cherrie, Callum Wilson, wote wakiwa na umri na 28. (Talksport)Aston Villa pia imeonesha nia ya kumsajili Wilson kutoka Bournemouth. (Mail)Schalke inamkodolea macho mlinda lango wa Arsenal Emiliano Martinez, 27, raia wa Argentina ambaye pia amehusishwa na Aston Villa. (Sky Sports)Arsenal imekubali kumtoa beki wa kati Rob Holding, 24, Newcastle United kwa mkopo na makubaliano hayo yanatarajiwa kukamilika wiki hii. (Talksport)Inter Milan huenda ikamuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, miezi minane baada ya kumsajili kutoka Tottenham. (Corriere dello Sport – in Italian)Crystal Palace inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher, 20, kwa mkopo. (Sun),

 Lionel Messi ataondoka Barcelona msimu hii na ” inawezekana” akaelekea Manchester City, kwa mujibu wa mgombea wa urais wa klabu hiyo, Toni Freixa. (Goal)

Barcelona inaamini kwamba njia pekee ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 33, kuondoka kihalali bure ni ikiwa ataahidi kwamba hatashiriki katika michuano ya msimu ujao.(ESPN)

Rais wa Argentina, Alberto Fernandez, amemshauri Messi kurejea katika klabu yake ya ujana ya Newell’s Old Boys. (C5N, via Evening Standard)

Chelsea imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, kwa kima cha kwanza cha pauni milioni 72, na kusababisha pesa za matumizi yao kipindi cha uhamisho kuongezeka hadi pauni milioni 200. (Guardian)

Manchester United inamlenga mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 21. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 24, anasemekana kwamba wiki hii atajiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Guardian)

Vilabu vya Saudi Arabia na Qatar vimeonesha nia ya kumsajili Mjerumani Mesut Ozil msimu huu lakini mchezaji huyo wa Arsenal, 31, hana nia ya kuondoka London. (Telegraph)

Tottenham imeanzisha mazungumzo ya mkataba mpya wa mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris, 33, licha ya kumsajili Joe Hart kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)

Spurs inafanya mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Joshua King na pia inamnyatia mshambuliaji Mwingereza wa Cherrie, Callum Wilson, wote wakiwa na umri na 28. (Talksport)

Aston Villa pia imeonesha nia ya kumsajili Wilson kutoka Bournemouth. (Mail)

Schalke inamkodolea macho mlinda lango wa Arsenal Emiliano Martinez, 27, raia wa Argentina ambaye pia amehusishwa na Aston Villa. (Sky Sports)

Arsenal imekubali kumtoa beki wa kati Rob Holding, 24, Newcastle United kwa mkopo na makubaliano hayo yanatarajiwa kukamilika wiki hii. (Talksport)

Inter Milan huenda ikamuuza kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, miezi minane baada ya kumsajili kutoka Tottenham. (Corriere dello Sport – in Italian)

Crystal Palace inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher, 20, kwa mkopo. (Sun)

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *