Tetesi za soka kimataifa,

October 2, 2020

 Tottenham wamekataa ofa ya mkopo wa pauni milioni 1.5 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya mlinda mlango Dele Alli na mchezaji huyo, 24, anajiandaa kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya London. (Guardian

Lakini klabu ya Ligue 1 watakuwa wanaandaa ofa ya mwisho ya mkopo kwa ajili ya Alli. (Telegraph)

Spurs pia imeweka ofa ya mkopo kwa ajili ya mlinzi Antonio Rudiger, 27, anayekipiga Chelsea, wakati mazungumzo yakiendelea kati ya mahasimu hao wa London. (Nicolo Schira via Express)

Antonio Rudiger alisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Mabara mwaka 2017 nchini Urusi

Arsenal wamekubali dili la mkopo kwa ajili ya mlinzi wa Uruguay Lucas Torreira, 24, kwenda Atletico Madrid, na hatua hiyo itawaruhusu kumsajili kiungo wa kati Hossem Aouar, 22, kutoka Lyon. (AS,via Mirror)

Inter Milan wanajiandaa kumnasa beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso, 29. (Sky Sports)

Leicester City inajiandaa kutoa ofa ya mkataba mpya kwa winga Harvey Barnes, 22. (Telegraph)

Inter Milan wanajiandaa kumnasa beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso,29. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain wanaweza kudhoofisha mpango wa washika bunduki kumshawishi Aouar baada ya pia kuingia kwenye mazungumzo ya kumnasaMfaransa huyo. (L’Equipe,via Metro)

Leicester City wako tayari kupokea ofa kwa ajili ya winga Demarai Gray, ambaye yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo. (Mirror)

Manchester United wanajaribu kumsajili winga wa Atalanta na Ivory Coast Amad Traore, 18. (Manchester Evening News)

Fulham wanajaribu kuwanasa mabeki wa kati wawili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili tarehe 5 mwezi Oktoba, huku klabu ikimfuatilia mlinzi wa PSV Eindhoven Timo Baumgartl, 24. (Telegraph)

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *