TCAA yakanusha madai, kuzuia helikopta ya CHADEMA, on September 11, 2020 at 6:00 am

September 11, 2020

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekanusha kuinyima kibali Helikopta iliyokuwa itumike na mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu katika mikutano yake ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu.Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo na mamlaka hiyo, imesema kuwa Helikopta hiyo imepewa kibali cha muda mrefu (block permit) na TCAA kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 31, 2020 na kukanusha madai hayo.Mkurugenzi Mkuu TCCA, Hamza Johari amekanusha pia uwepo wa ofisa wa mamlaka hiyo aliyetoa taarifa kuhusu safari ya msafara wa Mhe. Lissu  kutokuwepo kwani safari ya CHADEMA haikuwepo kwenye orodha. Ufafanuzi huo wa TCAA umekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene kuwa helikopta iliyokuwa itumike na Tundu Lissu ilizuiliwa na mamlaka hiyo.,

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekanusha kuinyima kibali Helikopta iliyokuwa itumike na mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu katika mikutano yake ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo na mamlaka hiyo, imesema kuwa Helikopta hiyo imepewa kibali cha muda mrefu (block permit) na TCAA kwa shughuli za kampeni za uchaguzi kuanzia Septemba 4 hadi Oktoba 31, 2020 na kukanusha madai hayo.

Mkurugenzi Mkuu TCCA, Hamza Johari amekanusha pia uwepo wa ofisa wa mamlaka hiyo aliyetoa taarifa kuhusu safari ya msafara wa Mhe. Lissu  kutokuwepo kwani safari ya CHADEMA haikuwepo kwenye orodha. 

Ufafanuzi huo wa TCAA umekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene kuwa helikopta iliyokuwa itumike na Tundu Lissu ilizuiliwa na mamlaka hiyo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *