TBC na Chadema Wamaliza Mgogoro Wao, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 5, 2020

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) jana Ijumaa Septemba 4, 2020 limefanikiwa kumaliza mgogoro uliokuwapo kati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC), baada ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi hizo jijini Dar es Salaam, leo Ijumaaa Septemba 4, 2020TEF kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake, Deodatus Balile ilifanya mawasiliano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayubu Ryoba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Willison Mahera Charles, ambao wamekutana leo katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam kumaliza mgogoro huo.Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera, wakati anafungua kikao hicho cha usuluhishi, amesema vyombo vya habari vya umma vinawajibika kutoa fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 53 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, sambamba na Maadili ya Uchaguzi, Katiba ya Tanzania, Sheria mbalimbali na maelekezo ya Tume.Pia amesema vyama vya siasa na wafuasi wao wanawajibika kutii sheria za nchini kwa kuhakikisha wanalinda amani na utulivu. Amevitaka vyama vya siasa kuepuka kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho kwenye mikutano ya kampeni.Katika mkutano huo Mwenyekiti wa TEF, Balile ameeleza umuhimu wa vyombo vya habari kushirikiana na vyama vya siasa kwa kutimiza wajibu wake wa kitaaluma, lakini pia akafafanua umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana na vyombo vya habari hasa kipindi hiki cha kampeni kupata fursa ya kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya sera za vyama vyao katika majukwaa ya siasa.Amevitaka vyama kukosoana bila kutumia lugha ngumu au kuingia katika ugomvi binafsi na watu au matusi hali inayovipa wakati mgumu vyombo vinavyorusha matangazo ‘live’.Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ryoba amelishukuru Jukwaa la Wahariri kwa juhudi za kuikutanisha TBC na Chadema, ila akaeleza masikitiko yake kuwa uamuzi wa Chadema kufukuza waandishi wao katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni, Mbagala wiki iliyopita ulikuwa unahatarisha maisha ya waandishi na mali za shirika.Pia amesema hatua ya Chadema ililenga kubomoa kiwango cha TBC kuaminika mbele ya jamii, suala ambalo ni gharama kubwa kwa chombo cha habari. Hata hivyo amekiri upungufu uliofanywa na watangazaji siku hiyo kwa jinsi matangazo yaliyokatwa na mjadala ulioendelea studio, hivyo akasema shirika litajitahidi kutorudia makosa yaliyojitokezaMwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza historia ya uhusiano wa TBC na Chadema kwamba kwa muda mrefu umekuwa si mzuri na akasema hata baadhi ya vyombo vya habari binafsi vinakataa kurusha matangazo ya shughuli za chama chao hata kama kinalipia kwa maelezo kuwa vimepewa maelekezo. Mbowe ameviomba vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sheria, hasa katika kipindi hiki cha kampeni.Baada ya mjadala mrefu, Dk. Ryoba na Mbowe walikubaliana kumaliza tofauti zao kwa kupeana mikono na kuahidi kurejesha ushirikiano. Mbowe amesema atawatangazia wanachama wa Chadema kuwa wako tayari kufanya kazi na TBC kuanzia sasa.Dk. Ryoba amesema Chadema wawapatie TBC ratiba ya mikutano yao watashiriki kikamilifu kuitangaza. Pia, amemwabia Mbowe kuwa TBC ina kipindi cha nusu saa kila wiki kwa wagombea kunadi sera zao kinachorushwa bila malipo, hivyo akawaalika Chadema kuitumia fursa hiyo, ambapo Mbowe amekubali kuitumia.Akifunga kikao, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, ameishukuru TEF kwa juhudi ilizofanya kuwakutanisha TBC na Chadema na akaviomba vyama vya siasa nchini kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.Dk. Ryoba, Mbowe, Dk. Mahera na Balile wamepeana mikono kuashiria kufungua ukurasa mpya na wakaahidi kumaliza migogoro kati ya vyombo vya habari na vyama vya siasa au wanasiasa nchini kwa njia ya mazungumzo badala ya kutegemea sheria pekee katika kipindi hiki cha uchaguzi.,

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) jana Ijumaa Septemba 4, 2020 limefanikiwa kumaliza mgogoro uliokuwapo kati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC), baada ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi hizo jijini Dar es Salaam, leo Ijumaaa Septemba 4, 2020

TEF kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake, Deodatus Balile ilifanya mawasiliano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayubu Ryoba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Willison Mahera Charles, ambao wamekutana leo katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam kumaliza mgogoro huo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera, wakati anafungua kikao hicho cha usuluhishi, amesema vyombo vya habari vya umma vinawajibika kutoa fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 53 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, sambamba na Maadili ya Uchaguzi, Katiba ya Tanzania, Sheria mbalimbali na maelekezo ya Tume.

Pia amesema vyama vya siasa na wafuasi wao wanawajibika kutii sheria za nchini kwa kuhakikisha wanalinda amani na utulivu. Amevitaka vyama vya siasa kuepuka kutoa tuhuma zisizo na uthibitisho kwenye mikutano ya kampeni.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa TEF, Balile ameeleza umuhimu wa vyombo vya habari kushirikiana na vyama vya siasa kwa kutimiza wajibu wake wa kitaaluma, lakini pia akafafanua umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana na vyombo vya habari hasa kipindi hiki cha kampeni kupata fursa ya kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya sera za vyama vyao katika majukwaa ya siasa.

Amevitaka vyama kukosoana bila kutumia lugha ngumu au kuingia katika ugomvi binafsi na watu au matusi hali inayovipa wakati mgumu vyombo vinavyorusha matangazo ‘live’.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ryoba amelishukuru Jukwaa la Wahariri kwa juhudi za kuikutanisha TBC na Chadema, ila akaeleza masikitiko yake kuwa uamuzi wa Chadema kufukuza waandishi wao katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni, Mbagala wiki iliyopita ulikuwa unahatarisha maisha ya waandishi na mali za shirika.

Pia amesema hatua ya Chadema ililenga kubomoa kiwango cha TBC kuaminika mbele ya jamii, suala ambalo ni gharama kubwa kwa chombo cha habari. Hata hivyo amekiri upungufu uliofanywa na watangazaji siku hiyo kwa jinsi matangazo yaliyokatwa na mjadala ulioendelea studio, hivyo akasema shirika litajitahidi kutorudia makosa yaliyojitokeza

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameeleza historia ya uhusiano wa TBC na Chadema kwamba kwa muda mrefu umekuwa si mzuri na akasema hata baadhi ya vyombo vya habari binafsi vinakataa kurusha matangazo ya shughuli za chama chao hata kama kinalipia kwa maelezo kuwa vimepewa maelekezo. Mbowe ameviomba vyombo vya habari kufanya kazi kwa weledi na kwa mujibu wa sheria, hasa katika kipindi hiki cha kampeni.

Baada ya mjadala mrefu, Dk. Ryoba na Mbowe walikubaliana kumaliza tofauti zao kwa kupeana mikono na kuahidi kurejesha ushirikiano. Mbowe amesema atawatangazia wanachama wa Chadema kuwa wako tayari kufanya kazi na TBC kuanzia sasa.

Dk. Ryoba amesema Chadema wawapatie TBC ratiba ya mikutano yao watashiriki kikamilifu kuitangaza. Pia, amemwabia Mbowe kuwa TBC ina kipindi cha nusu saa kila wiki kwa wagombea kunadi sera zao kinachorushwa bila malipo, hivyo akawaalika Chadema kuitumia fursa hiyo, ambapo Mbowe amekubali kuitumia.

Akifunga kikao, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Mahera aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, ameishukuru TEF kwa juhudi ilizofanya kuwakutanisha TBC na Chadema na akaviomba vyama vya siasa nchini kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.

Dk. Ryoba, Mbowe, Dk. Mahera na Balile wamepeana mikono kuashiria kufungua ukurasa mpya na wakaahidi kumaliza migogoro kati ya vyombo vya habari na vyama vya siasa au wanasiasa nchini kwa njia ya mazungumzo badala ya kutegemea sheria pekee katika kipindi hiki cha uchaguzi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *