‘Tayari Bill keshazingua nini?,’Mashabiki wamuuliza Nandy baada ya kuposti ua jeusi

October 2, 2020

Msanii wa nyimbo za bongo Faustina Charles Mfinanga almaarufu Nandy amewaacha mashabiki wake midomo wazi na hata kama wamechanganyikiwa baada ya kuposti ua jeusi kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika maelezo mafupi ya kuwa moyo uliovunjika.

“Moyo uliovunjika.” Aliandika Nandy.(Heartbroken).

Nandy amekuwa akimpigia rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kampeni za kuwa rais tena, watu mashuhuri wamekuwa wakitumia ua hilo kuonyesha kuwa uhusiano wao wa kimapenzi umekwisha.

Miezi michache iliyopita, mpenzi wake Nandy Rappa Bill Nass alimchumbia mwanamuziki huyo, huku akimvisha pete hadharani na kusema haya.

“We’ve been together kwa kipindi kirefu sana tumepitia vitu vingi vizuri na vibaya. Najua upande wako mbaya, najua upande wako mzuri but nimechagua pande zote mbili nakupenda sana na ninatamani dunia nzima ijue so leo itakuwa siku nzuri sana kupropose. I love you.” Bill Alizungumza.

Ni posti ambayo iliibua hisia tofauti, hizi hapa hisia za mashabiki wake;

dessy_a7: Tayari billnass Kashazingua nini? 😂😂😂 au nyimbo

princeanwarguzm: Kiki ya nyimbo mpyaaaa naona anataka kutoa nyimb

_mack24: Bill Nasi kafanya nini tena huko😂😂😂

glory_trisher: Kumekucha ushaacha mty

mamumossatz9: Mmeshaanza na nyie msituchoshe. Ila hata mimi ningekuwa ndio billinas sikuoi kwa maneno yale ya mama yako na dada yako wallah navunja uchumba

wema_memes: Mungu wanguuu Kwan ni niniiii

Nandy 

Nandy

celebrities.judge: Em usituchoshe nawewe Kwan utakua wa kwanza kuachika

miss_shamsah: Wanapenda kutuchanganya🤣🤣🤣

mlitomariamu: Jmn uwa jeusi tena mmmh mwa2tisha mbona mlitamba sana tayari mshaachana wanadam hawa si wa2 wazuri😀😀😀😀

officialnombo: Kale kawimbo Kakivuruge Tayari Kanaingia Kwenye Uhisika ☺️

Photo Credits: hisani

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *