Tatizo linalomsibu MB Dogg hadi kuhamia Mpakani

September 12, 2020

 Staa wa BongoFleva aliyetamba na ngoma ya ‘Latifa’ na ‘si uliniambia’ MB Dogg ameeleza kuwa pesa na sapoti ndiyo changamoto ambayo inamsumbua kwa sasa hadi kuhama mji kufanya shughuli zake nje ya Dar Es Salaam.Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital kuhusu ukimya wake MB Dogg amesema kazi ya muziki haiwezi akiwa peke yake hivyo anahitaji msaada, sapoti na pesa.”Biashara ya muziki imekuwa na changamoto kubwa ambapo watu wanawekeza sana kwenye kuwezesha, ukijikuta upo mwenyewe halafu una mipango mingi itabidi utafute watu wakukingie kifua, sapoti na pesa ambayo inahitajika japo sio sana ila ndiyo kikwazo kikubwa kingine ni nguvu na akili”Aidha MB Dogg ameongeza kusema kuna harakati ambazo anazifanya kwa sasa zinazosababisha kuhama mji na sasa hivi anafika hadi boda ya Holoholo ambapo ni mpakani mwa Tanzania kuingia Mombasa, Kenya ili kukamilisha shughuli hizo.,

 
Staa wa BongoFleva aliyetamba na ngoma ya ‘Latifa’ na ‘si uliniambia’ MB Dogg ameeleza kuwa pesa na sapoti ndiyo changamoto ambayo inamsumbua kwa sasa hadi kuhama mji kufanya shughuli zake nje ya Dar Es Salaam.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital kuhusu ukimya wake MB Dogg amesema kazi ya muziki haiwezi akiwa peke yake hivyo anahitaji msaada, sapoti na pesa.

“Biashara ya muziki imekuwa na changamoto kubwa ambapo watu wanawekeza sana kwenye kuwezesha, ukijikuta upo mwenyewe halafu una mipango mingi itabidi utafute watu wakukingie kifua, sapoti na pesa ambayo inahitajika japo sio sana ila ndiyo kikwazo kikubwa kingine ni nguvu na akili”

Aidha MB Dogg ameongeza kusema kuna harakati ambazo anazifanya kwa sasa zinazosababisha kuhama mji na sasa hivi anafika hadi boda ya Holoholo ambapo ni mpakani mwa Tanzania kuingia Mombasa, Kenya ili kukamilisha shughuli hizo.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *