Tasuba yakabiliwa na changamoto ya majengo, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on August 30, 2020 at 10:00 am

August 30, 2020

Na Omary Mngindo, Bagamoyo.TAASISI ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya kufundishia ikiwemo uchakavu wa majengo.Aidha kutokana na upungufu huo wanachuo wanalazimika kuishi nje ya maeneo ya taasisi, hali inayowaathiri kwa kiasi kikubwa kitaaluma, kiusalama na kimaadili hali inayochangiwa na uchakavu wa mabweni, huku ikielezea imani yao kwa mgeni rasmi katika Mahafali yao.Hayo yamo katika taarifa ya Wahitimu 59 wa miaka miwili ya masomo chuoni hapo, mbele ya Mgeni rasmi boubakary Mlawa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo, iliyisomwa na mmoja wa wahitimu Anjela Mhilu, ambayo imeelezea changamoto mbalimbali.”Chuo kinakabiliwa na uchakavu wa mabweni hali inayotulazimu wanafunzi kuishi nje ya chuo, pia tunahitaji kompyuta, machine ya kuchapisha (Printa), Photocopy Mashine na akana,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Emmanuel Bwire alimwelezea mgeni rasmi kwamba changamoto hizo kwa namna moja au nyingine zinakwamisha juhudi za walimu kufundisha na wanafunzi kupokea mafunzo, huku akimuomba mgeni rasmi afikishe kwa viongozi wa juu.Akizungumza na wahitimu hao, Mlawa alianza kuupongeza uongozi wa shule kwa namna wanavyokabiliana na changamoyo hizo lakini wanaendelea kuwapatia elimu wanafunzi, huku akiahidi kuzifikisha Serikali zilizo nje ya uwezo wake.”Kwa niaba ya Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo mimi ndio Mwenyekiti, katika hizi changamoto kuna baadhi zipo ndani ya uwezo, tutandaa chakula cha Hisani kwa ajli ya kupata fedha za kukarabati mabweni yetu,” alisema Mlawa.Aidha aliongeza kwamba kati ya changamoto hizo hizo nyingine atazifikisha kwa uongozi wa juu ili ziweze kufanyiwakazi, huku akieleza kuwa serikali ya awamu ya Tano chini.ya Rais Dkt. John Magufuli inathamini sana elimu.”Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu mpendwa John Magufuli inafanyakazi kubwa, sote ni mashahidi, kati ya hizi changamoto zipo tutazozikabili wenyewe kwa kuandaa chakula cha jioni, zilizo juu ya uwezo wetu tutazifikisha kwa viongozi wetu ngazi za juu,” alisema Mlawa.,

Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya kufundishia ikiwemo uchakavu wa majengo.

Aidha kutokana na upungufu huo wanachuo wanalazimika kuishi nje ya maeneo ya taasisi, hali inayowaathiri kwa kiasi kikubwa kitaaluma, kiusalama na kimaadili hali inayochangiwa na uchakavu wa mabweni, huku ikielezea imani yao kwa mgeni rasmi katika Mahafali yao.

Hayo yamo katika taarifa ya Wahitimu 59 wa miaka miwili ya masomo chuoni hapo, mbele ya Mgeni rasmi boubakary Mlawa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo, iliyisomwa na mmoja wa wahitimu Anjela Mhilu, ambayo imeelezea changamoto mbalimbali.

“Chuo kinakabiliwa na uchakavu wa mabweni hali inayotulazimu wanafunzi kuishi nje ya chuo, pia tunahitaji kompyuta, machine ya kuchapisha (Printa), Photocopy Mashine na akana,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Emmanuel Bwire alimwelezea mgeni rasmi kwamba changamoto hizo kwa namna moja au nyingine zinakwamisha juhudi za walimu kufundisha na wanafunzi kupokea mafunzo, huku akimuomba mgeni rasmi afikishe kwa viongozi wa juu.

Akizungumza na wahitimu hao, Mlawa alianza kuupongeza uongozi wa shule kwa namna wanavyokabiliana na changamoyo hizo lakini wanaendelea kuwapatia elimu wanafunzi, huku akiahidi kuzifikisha Serikali zilizo nje ya uwezo wake.

“Kwa niaba ya Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo mimi ndio Mwenyekiti, katika hizi changamoto kuna baadhi zipo ndani ya uwezo, tutandaa chakula cha Hisani kwa ajli ya kupata fedha za kukarabati mabweni yetu,” alisema Mlawa.

Aidha aliongeza kwamba kati ya changamoto hizo hizo nyingine atazifikisha kwa uongozi wa juu ili ziweze kufanyiwakazi, huku akieleza kuwa serikali ya awamu ya Tano chini.ya Rais Dkt. John Magufuli inathamini sana elimu.

“Serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu mpendwa John Magufuli inafanyakazi kubwa, sote ni mashahidi, kati ya hizi changamoto zipo tutazozikabili wenyewe kwa kuandaa chakula cha jioni, zilizo juu ya uwezo wetu tutazifikisha kwa viongozi wetu ngazi za juu,” alisema Mlawa.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *